Zawadi 5 kila dereva uber anapewa

ZAWADI 5 KILA DEREVA UBER ANAPEWA NA KAMPUNI

Je unazifahamu zawadi 5 kila dereva Uber hupewa mara tu anapojiunga kuendesha abiria kwenye jukwaa hili la usafiri?

Uber ni moja ya kampuni zinazoongoza katika sekta ya usafiri kwa njia ya programu duniani. Tangu ipate mafanikio makubwa, zimeibuka kampuni nyingine ambazo zimekuwa zikijaribu kushindana na Uber ili nao wapate mafanikio makubwa.

Kutokana na ushindani huu, Kampuni ya Uber imekuwa ikijitahidi sana kujaribu kuridhisha madereva wake ili kuhakikisha hawahami na kwenda kujiunga na kampuni nyingine.

Katika makala hii utaenda kuona zawadi au motisha aina 5 ambazo Uber inawapa madereva wake ili kuwasaidia kupata hela zaidi na kupunguza gharama za uendeshaji.

ZAWADI 5 KILA DEREVA UBER ANAPEWA NA KAMPUNI.

1. BIMA YA AJALI BURE!

Kampuni ya Uber imeingia ubia na kampuni mbalimbali za bima duniani kukata bima za ajali kwa ajili ya madereva wote pamoja na abiria.

Kwa hapa Tanzania Uber ikishirikiana na kampuni ya Britam insurance inatoa bima za aina mbili kwa ajili ya madereva.

  • 3rd party comprehensive insurance kwa bei punguzo: Hii ni bima ambayo fidia inalipwa kwa mtu mwengine ambaye wewe umesababisha ajali na uharibifu wa gari lake au afya yake. Madereva wa Uber wakikata bima hii gharama yake inakuwa ndogo kwasababu Uber imeingia ubia na Britam.
  • Bima ya Afya: Kama hauna bima hii basi kama dereva wa Uber una nafasi ya kupata huduma hii kwa bei ndogo ya kuanzia 89,000/= tsh tu! Bei hii ni tofauti na kampuni nyingine za bima ambazo Uber haina mahusiano nayo.
  • Bima ya majeraha: Kila dereva Uber anapokubaliwa kuanza biashara ya kuendesha abiria anakuwa amekatiwa bima ya ajali bure na kampuni. Hata kama tayari una bima na kampuni nyingine au kama bima yako ya biashara inajumuisha majeraha ya ajali, bima ya Uber inakulinda zaidi na kuhakikisha dereva unalipwa fidia unapoumia, kupata ulemavu na familia zinapewa fidia kama kwa bahati mbaya dereva anafariki kwa ajali akiwa anaendesha.

Vipo vigezo vingi vya kueleweka tu vya jinsi bima hii inavyolinda madereva. Unaweza kutembelea ofisi za Uber kwa ajili ya maelekezo zaidi.

Au soma makala hii inayoichambua bima hii kiundani zaidi.

2. MKOPO WA SIMU

Kuwa dereva Uber ni muhimu kuwa na simu janja yenye viwango vya kuridhisha kwasababu jukwaa la Uber limetengenezwa kwa teknolojia za viwango vya juu.

Moja ya changamoto wanazopata madereva Uber ni app kuganda, na hili tatizo huwa linaweza kuletwa na ubora mdogo wa simu. Ili kupunguza na kuepusha tatizo hili, kampuni ya Uber iliingia ubia na duka maarufu la simu za mkononi ili kusaidia kila dereva apate simu janja yenye viwango vya hali ya juu kwa bei pungufu.

Duka la Simkopo linasaidia wanunuaji kuweza kununua simu na kulipia kidogo kidogo kwa muda fulani kutokana na makubaliano ya mnunuzi.

Kwa miaka mingi huduma hii imekuwa ikisaidia watu wengi kupata simu makini ambazo wasingeweza kupata kama ingebidi kununua sehemu nyingine kwa pesa kamili yaani cash.

Duka linapatikana Bimaport, Jangid Plaza, Chabruma St, Dar es salaam, au unaweza kuwatafuta kupitia namba:

Kila dereva aliyesajiliwa kuendesha anaweza kwenda dukani na kujipatia simu janja ya viwango vya hali ya juu kwa discount na kwa kulipa kwa awamu.

Tembelea ofisi za Uber ili kupata maelekezo zaidi na ujisajili kabla ya kwenda kupata simu yako ili kuhakikisha muda wote app yako ipo hewani bila hitilafu zozote.

Fahamu ofisi za Uber zilipo na namba zao za simu kupitia makala hii.

3. Jerry Spare Parts

Zawadi ya 3 kati ya zawadi 5 kila dereva Uber anapewa na kampuni ni punguzo la hadi 50% kwa huduma za kutengeneza magari.

Jerry spare parts ni moja ya kampuni zinazoongoza katika kuuza spare za magari za viwango vya juu kutoka nje ya Afrika. Wewe kama dereva Uber utapata punguzo kubwa utakapoenda kupata huduma ya kubadili oil au filter ya mafuta.

Pia utapata punguzo kubwa unaponunua baadhi ya spare au unapohitaji huduma ya ufundi.

Garage hii inapatikana Victoria Dar es salaam pamoja na Unga limited Arusha. Unaweza kuwapata kwa namba zifuatazo lakini tembelea ofisi za Uber Greenlight Hub ili ku-book huduma kabla ya kwenda garage.

4. UTRACK AFRICA LIMITED

Kampuni ya Uber imeingia ubia na moja ya kampuni zinazoongoza katika kusambaza bidhaa na huduma za usalama wa magari kwa kutumia gps tracking.

Kampuni hii inatumiwa na makampuni makubwa Afrika mashariki nzima kwa ajili ya kuweka gps kwenye magari yao ya kusafirisha bidhaa mbalimbali.

Pia inatumiwa na idara mbalimbali zaa serikali katika kuhakikisha usalama na ufuatiliaji wa magari ya serikali wakati wote.

Kutokana na ushirikiano na kampuni ya Uber, madereva wanaweza kupata huduma na vifaa hivi vya kulinda magari yao kwa bei ndogo zaidi kuliko wengine. Kwa kuanzia 37,000/=tsh tu kwa mwezi dereva Uber unaweza kupata vifaa vya kufatilia gari lako lilipo hivyo kukupa amani kuwa utalipata pale ambapo linaweza kuibiwa.

Soma zaidi kuhusu utrack Africa Limited kwa kubonyeza hapa.

5. MIKOPO MIDOGO

Ya mwisho katika zawadi 5 kila dereva Uber anapewa ni uwezo wa kupata mkopo kwa ajili ya kuboresha huduma zao za uendeshaji.

Uber ikishirikiana na kampuni ya Platinum Credit Limited kupitia huduma ya jibusti inatoa mkopo wa hadi milioni moja ndani ya masaa mawili tu kwa madereva.

Mkopo ni haraka na gharama ndogo ya nyongeza wakati wa kulipia. Ili kupata mkopo wako tembelea ofisi za Uber kupata taarifa zaidi na kuanza mchakato.

Tembelea kurasa wa facebook wa Platinum credit Ltd ili kusoma zaidi jinsi ya kupata mkopo.

BONUS:

Uber imeingia ubia na msambazaji wa vinywaji laini au soft drinks kwa ajili ya kugawa vinywaji na maji katika ofisi zake. Kwa hiyo madereva wote wanaweza kupata wakiwa wanasubiri mtu wa kuwahudumia.

Kampuni ya Uber imekuwa na washindani wengi sana na wengine wataendelea kuongezeka. Hivyo ni kawaida kwamba wataendelea kutoa motisha mbali mbali ili madereva wake wasihame.

Tuambie kwenye comment section kama ulikuwa unafahau kuhusu hizi zawadi 5 kila dereva Uber anatakiwa apate. Kama umewahi kuzipata au kama utajaribu kuzipata.

Hakikisha unatembelea Weibak Carsharing website na kurasa zetu za social media ili kupata taarifa zote za haraka za maboresho na motisha zaidi!

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *