Wasiliana na uongozi wa uber

WASILIANA NA UONGOZI UBER KWA KUFATA NJIA HIZI

Uber ni jukwaa maarufu ambapo madereva na wamiliki vyombo vya usafiri huunganishwa na watu wenye hitaji la usafiri.

Kampuni hii ilianzishwa mwezi March mwaka 2009, San Francisco, California, Marekani. Hadi mwaka 2021 huduma za Uber zimefikia zaidi ya nchi 85, huku ikiweza kutoa fursa kwa madereva zaidi ya milioni 3-4 dunia nzima kutengeneza kipato kizuri sana.

Mwezi juni 15 mwaka 2016 Uber ilizindua shughuli zake jijini Dar es salaam Tanzania na kulifanya jiji hili kuwa jiji la 475 kutumia jukwaa la Uber kwa usafiri. Tangu hapo hadi leo hii maelfu ya madereva na wamiliki magari wamekuwa wakitengeneza kipato kikubwa kupitia huduma ya usafirishaji.

Fahamu jinsi ya kujisajili kuendesha Uber na we uwe miongoni mwa wanafaidikaji wa fursa hii!

JINSI YA KUWASILIANA NA UONGOZI WA UBER (HUDUMA KWA WATEJA)

Kama tayari wewe ni dereva katika jukwaa hili basi utakuwa tayari unafahamu kuwa si rahisi sana kupata mtu kutoka Uber wa kuongea naye na kukutatulia matatizo mapema.

Pata dondoo kutoka Weibak:

Lengo letu kuu ni kusambaza elimu ya kitaalamu kuhusu sekta ya usafiri huu wa jumuiya kwenye majukwaa ya Ride-sharing/Ride-hailing.

Hapa utapata taarifa up to date zitakazosaidia kuepuka changamoto, kuzisuluhisha na kukufanya utengeneze kipato kikubwa zaidi.

Katika makala hii tunaenda kukufafanulia njia 5 za uhakika zitakazokusaidia ku wasiliana na uongozi Uber Tanzania Limited ili uweze kutatua changamoto na kuendelea na shughuli za kutengeneza pesa..

1. WEBSITE YA UBER

Kabla ya kuanza kutafuta mtu wa kuongea naye Uber wanapendelea watumiaji kutembelea tovuti yao na kusoma makala mbalimbali zenye kuchambua matatizo na maswali mengi ambayo watumiaji huwa wanasumbuliwa nayo.

BONYEZA HAPA kuelekea kwenye sehemu maalumu ya website ya Uber, kisha pitia topics zilizoorodheshwa. Ukiona suala lako lipo kwenye orodha bonyeza kisha usome maelekezo na jinsi ya kujinasua.

Mara nyingi ni bora kutafuta suluhisho kupitia maelekezo ya kina yaliyopo kwenye tovuti hii kwasababu wanaoandika hivi makala wanafahamu maswali ambayo yanaulizwa sana na wanajua kwa kina jinsi ya kuyatatua.

Hii inaokoa muda kuliko kutafuta customer care ambaye atahitaji kwenda kuulizia suala lako kwasababu hawawezi kukumbuka kila suluhisho muda wote.

2. APP YA UBER

Kama una maswali na majibu haujapata kwenye website au kama vile una matatizo mfano kuhusu nauli, njia nzuri zaidi ya kupata utatuzi ni kupitia kipengele cha “MSAADA”/”HELP” kwenye app yako.

Kipengele hiki kinapatikana kwa kubonyeza menu ambayo ni alama ya mistari mitatu sehemu ya juu upande wa kushoto wa app ya Uber. Ukishabonyeza chagua “HELP” kisha pitia topic zote kuona kama ipo yenye kuongelea jambo lako.

Kama tatizo lako halipo kwenye list basi endelea kuchunguza hado ufike kipengele cha “Contact suppot” na uchague kutuma ujumbe au kuweka appointment ya kwenda ofisini kwao.

3. OFISI ZA UBER TANZANIA

Njia nyingine nzuri ya ku wasiliana na uongozi Uber ni kutembelea ofisi zao. Ingawa Jukwaa la Uber linatoa huduma katika mji wa Dar es salaam, ofisi zao zipo Dar es salaam tu katika maeneo yafuatayo.

OFISI KUU

Ofisi za makao makuu ya Uber Tanzania zinapatikana Viva Towers Floor 1, Ali Hassan Mwinyi Road, Dar es salaam.

OFISI NDOGO

Uber Tanzania Limited ina pia ofisi ndogo iliyopo barabara ya Rose Garden. Hakuna taarifa kamili mtandaoni kuhusi saa za kazi za ofisi hizi. Ipo mahali inaonesha kuwa ofisi ya Rose garden ipo wazi masaa 24 huku ya Viva towers ikitajwa kuwa wazi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku.

PATA DIRECTIONS

Je mtu yeyote tu anaruhusiwa kutembelea ofisi hii?

Jibu ni hapana. Kama wewe ni dereva wa gari Uber basi hauruhusiwi kwenda kupata msaada katika ofisi hii. Wanaohudumiwa hapa ni madereva Bajaji na piki piki (boda boda) tu!

Hii ni kwasababu ya sheria iliyopo hivi sasa ambayo inazuia aina hizi za vyombo vya usafiri kuingia mjini ambapo ofisi kuu ndipo ilipo.

Kuanzia janga la uviko 19 lipambe moto, hairuhusiwi kwenda tu kwenye ofisi za Uber bila kufanya appointment kwanza kupitia ile menu ya kwenye app kama tulivyojadili hapo mwanzo.

Kwa kifupi bado Uber Tanzania Limited haijachukua nafasi ya kuandika muda maalum ambao ofisi zao zipo wazi. Taarifa zote zilizopo si maalumu, bali zimepatikana kutokana na maoni ya watu waliowahi kwenda.

Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kwenda na kutopata huduma siku hiyo.

4. NAMBA ZA SIMU

Kama unaishi nje ya Dar es salaam au kama unataka kuepuka kufunga safari hadi ofisini na kukosa huduma unaweza kuwasiliana na uongozi Uber kupitia simu yako ya mkononi.

Uber Tanzania Limited mini office ya Rose garden haijafafanua muda wa kazi lakini namba yake ya simu imewekwa ifuatayo ambayo inapatikana masaa 24.

Pia kutikana na taarifa za kwenye BLOG HII Kampuni ya Uber ina huduma za usalama(security) masaa 24. Endapo dereva au abiria anapohisi yupo kwenye hatari na anahitaji msaada anaweza kupata msaada kwa namba zifuatazo

Tutaendelea kuedit na kuboresha makala hii pale ambapo namba nyingine za simu za kuwasiliana na uongozi Uber zitakapotajwa. Kwa hiyo usiondoke kwenye website hii bila kujisajili kupata dondoo za kila wiki!

5. KURASA ZA MITANDAO YA KIJAMII.

Moja ya njia nzuri na fanisi ya kuwasiliana na customer care wa makampuni ya usafiri ni Kuwatumia ujumbe kupitia kurasa zao za kwenye mitandao ya jamii.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba Uber Tanzania Limited haina tena kurasa hizi kama hapo zamani. Hii ni tofauti na kampuni nyingine kwa mfano Bolt ambayo unaweza kuwasilisha tatizo lako hata sehemu ya komenti za kurasa zao za Facebook, Instagram au hata twitter.

Soma hapa jinsi ya kujisajili kuwa dereva wa Bolt.

Kwa kifupi: njia Bora zaidi ya ku wasiliana na uongozi Uber ni kupitia website yao ya Help.uber.com. Kama bado tatizo lako halijapata utatuzi basi hatua inayofata ni kwenda kwenye menu ya app kwenye simu yako na kutafuta kipengele cha “HELP

Hapa napo ukikosa suluhu basi book appointment uende moja kwa moja ofisini kwao au jaribu kuwapigia simu na kusuluhisha jambo lako.

1 thought on “WASILIANA NA UONGOZI UBER KWA KUFATA NJIA HIZI”

  1. Pingback: BIASHARA YA UBER INALIPA KWELI KWA TANZANIA 2022?

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *