Wasiliana na uongozi Bolt

WASILIANA NA UONGOZI BOLT TANZANIA KWA NJIA ZIFUATAZO

Kama wewe tayari ni dereva uliyesajiliwa kuendesha abiria ni muhimu kufahamu njia hizi unapotaka ku wasiliana na uongozi Bolt ili kupata huduma za ziada.

Sababu zinazoweza kusababisha uhitaji wa kuwasiliana na uongozi.

1. KUPATA MAFUNZO YA MADEREVA

Kampuni ya Bolt imejikita sana katika kuhakikisha madereva wote wanapata mafunzo maalumu ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa ufanisi wa hali ya juu.

Mafunzo haya hutolewa ana kwa ana katika vituo maalumu ambavyo ni ofisi za Bolt. Kwa hiyo ili kuhakikisha dereva haukosi kuhudhuria, ni vizuri kuwasiliana na uongozi ili kujua tarehe muda na eneo la tukio.

2. KUPATA STIKA YA BOLT

Mara nyingi magari yenye stika ya nembo ya Bolt hupendelewa zaidi na abiria kwasababu inawafanya kumuamini zaidi dereva kuliko tu kuingia kwenye gari la mtu lisilokuwa na nembo.

Dereva unaweza kutembelea ofisi za Bolt au kuongea na muhudumu wa huduma kwa wateja ili kupata maelekezo sahihi ya kupata stika yako.

3. KUWASILISHA MALALAMIKO

Ili kupata huduma ya haraka ya kutatuliwa matatizo ni muhimu kuwa na mawasiliano sahihi hasa namba za simu na direction za ofisi.

Malalamiko ambayo ni rahisi zaidi kutatuliwa kwa kuongea na mtu wa huduma kwa wateja ni kama madai ya nauli, kutoa taarifa za ajali au kufunguliwa kwa akaunti ya dereva iliyofungwa kimakosa na malalamiko mengine.

NJIA ZA KU WASILIANA NA UONGOZI BOLT TANZANIA 2022

1. KUTUMA EMAIL KWA CUSTOMER SUPPORT

Kampuni ya Bolt ina anwani ya barua pepe maalumu kwa madereva wanaohitaji usaidizi wa mtu wa huduma kwa wateja.

Zifahamu sheria za utoaji huduma Bolt.

Kwa ajili ya kuuliza maswali au kupata msaada wowote kutoka kwa uongozi wa Bolt Tanzania tuma barua pepe kwenda moja ya anwani hizi kulingana na jiji ulilojisajilia kuendesha abiria:

[email protected]

[email protected]

[email protected]

[email protected]

Madereva wapya ambao bado hawajasajiliwa wanaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja kupitia anwani ifuatayo:

[email protected]

[email protected]

[email protected]

[email protected]

2. TEMBELEA OFISI

Tofauti na Uber, kampuni ya Bolt ina ofisi zake katika kila jiji ambalo inaendesha shughuli zake. Hii inasaidia sana kuleta usawa katika kutoa huduma.

Mara nyingi kampuni hizi za ride hailing hufungua ofisi katika jiiji kubwa tu hivyo kuacha wale madereva waliopo nje ya Dar es salaam kukosa huduma za ana kwa ana.

Zifuatazo ni sehemu ofisi za Bolt zilipo.

Ofisi ya Bolt Dar es salaam

Kampuni ya Bolt ina ofisi nyumba namba 4, mtaa wa Uzima, Mikocheni kwa Nyerere. Unaweza kuwa tembelea na kupata huduma za kiofisi kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja kamili jioni.

Mafunzo ya madereva hutolewa katika ofisi hizi kuanzia jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nane mchana.

Ofisi za Bolt Dodoma

Kampuni ya Bolt ina ofisi katika ghorofa la kwanza kwenye jengo la Capital City mall-Kisasa Petrol station Dar es salaam road Dodoma. Unawezakuwa tembelea na kupata huduma kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja kamili jioni.

Ofisi za Bolt Mwanza

Tembelea Rock city Mall, WING C ghorofa ya tatu ili kufika katika ofisi za Bolt kwa jiji la Mwanza. Ofisi zipo wazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hadi saa sita mchana kwa ajili ya kupata mafunzo ya madereva.

SOMA HAPA: Jinsi ya kutengeneza pesa nyingi kupitia jukwaa la Bolt.

3. KURASA ZA MITANDAO YA JAMII

Bolt Tanzania ni moja ya kampuni za ride hailing ambazo zina kurasa za mitandao ya jamii ambazo zipo active na zina wahudumuu wanao-update posti na kujibu comments.

Bila shaka unaweza kupata jibu haraka sana kwa kuwasilisha jambo lako moja kwa moja kwenye inbox au hata kwa kuacha ujumbe kwenye post mpya.

Hii ni moja ya quality nzuri sana ya Bolt ukilinganisha na kampuni nyingine kama Uber. Ingawa comment nyingi kwenye kurasa zao za mitandao ni za malalamiko, bado Bolt hawafuti message za watu wala hawakwepi kujibu maswali magumu.

Wasiliana na uongozi wa Bolt kwa kuwatumia ujumbe kwenye kurasa za zifuatazo:

Facebook: @Bolt

Twitter @Boltapp_tz

Instagram: @Bolt_tanzania

4. KUPITIA APP YA DEREVA

Wasiliana na uongozi Bolt kwa kupitia app yako kwa njia kuu mbili.

A:

 • Kwenye menu ya app yako nenda kwenye “Trips”
 • Chagua safari ambayo unataka kuripotia matatizo
 • Utatokea kwenye kipengele cha “Need help?” ambacho kina maswali mbalimbali ambayo huulizwa mara kwa mara.
 • Chagua swali ambalo linaendana na swali ulilonalo kisha libonyeze.
 • Utapelekwa kwenye makala yenye maelekezo ya swali hilo. Mwisho kabisa wa maelekezo utapata nafasi ya kuchagua kutuma ujumbe kwa huduma kwa wateja kwa ajili ya kupata utatuzi kutoka kwao.

B:

 • Kwenye Menu ya app ya dereva nenda kwenye “News”
 • Chini ya kipengele cha news utakuta makala za maswali yanayoulizwa mara kwa mara (Frequently asked questions au FAQ’s)
 • Tafuta swali ambalo linaendana na shida uliyonayo
 • Chagua kutuma ujumbe ili upate kuunganishwa na mtu wa huduma kwa wateja.

Bonyeza kitufe cha SOS kwa zaidi ya sekunde 3 ili kutuma ishara ya hatari/ kuhitaji msaada kwa Bolt pale unapokumbwa na hatari ya dharura. Hii itasaidia Bolt kukutrack ulipo na kuweza kuarifu maaskari waje kukusaidia.

TATIZO LA HITILAFU ZA NAULI

Kama shida yako ni nauli basi hakikisha unatuma fomu hii ya ukaguzi wa nauli kabla haujakubali au ku-confirm gharama ya safari.

5. KUPITIA TOVUTI YA BOLT

Unaweza ku wasiliana na uongozi Bolt kupitia ukurasa wa msaada katika tovuti ya Bolt.

Bonyeza hapa: kuelekea moja kwa moja

Ukilinganisha kampuni ya Bolt na Uber ni rahisi zaidi kupata customer care wa Bolt kuliko wa Uber. Hii ni kwasababu Bolt wamejikita katika kuupdate kurasa zao za mitandao ya jamii na kujibu comment za wadau wao.

Umewahi kupata shida hadi ukahitaji kuongea na mtu wa huduma kwa wateja wa Bolt? Ilikuwaje? uliridhika na huduma au la?

Tushirikishe katika comment ili sisi pamoja na jumuiya yetu ya madereva tuweze kujifunza na kuongeza ujuzi.

19 thoughts on “WASILIANA NA UONGOZI BOLT TANZANIA KWA NJIA ZIFUATAZO”

 1. Dereva wenu mussa nimemrikweti kaniambia nitembee toka kariakoo mtaa wa sikukuu.nimefika akaja akanipita na nilipompigia kaniambia hawezi rudi na akawahi kunikatia simu.nimeudhika sanaaaa. Huu ni uhuni

  1. Habari Mary, Pole sana kwa usumbufu ulioupata.

   Ila tungependa kukushauri uwasiliane moja kwa moja na uongozi wa kampuni husika kwa kutumia njia zilizowekwa kwenye makala hii kwani wao ndio wanahusika na huduma zote zinazotolewa na madereva wao. Sisi Weibak hatuhusiki na huduma zinazotolewa na kampuni hizi za usafirishaji, ila tumejikita katika kutoa huduma kwa madereva wa programu za safari na wamiliki wa magari. Tunatumai ukiwasiliana nao utapata msaada unaohitaji.

   Asante sana.

 2. Habari mimi ni abiria nina malala miko kwa mfano nataka kwenda sehemu kwenye cm yangu imesoma nauli 3000 lakini dereva akinifikiaha hiyo sehemu anasema 5000 naomba ufafanuzi hapo

  1. Habari Adalia, kwenye hili ni bora upate mchanganuo wa nauli unakuwaje. Mchanganuo wa nauli kwa trip yako unaweza upata moja kwa moja kupitia app au hata kwa njia ya barua pepe.

   Na next time unaweza subiri mpaka bei isome kwenye simu app yako.

 3. Nashida nimelipa kwa bolt tokea juzi lakini bado wameniachi Deni naomba msaada kwenye hio huduma maaana ntashindwa kufanya kazi namba yangu ya simu Ni 0654808539 ahsante

 4. Habari kuna dereva wenu wa bolt ni tapel kama sio mwizi nilisahau begi langu kweny bajaji yake nikampigia akaniambia lipo nimpigie nikirudi maan nilikua nasafr nimerudi kila nikimpigia sim hapokei wakT mwingn anakata na wala hajib sms naombeni msaada

  1. Habari Jackline! Pole kwa changamoto yako. Tunakushauri uwasiliane na kampuni husika ili waweze kukutatulia shida yako. Sisi Weibak sio teksi mtandao ila tumejikita katika kutoa taarifa zinazo waelimisha madereva na wamilki wa magari.

 5. habari.. nili patwa na dharula gariyangu ili ibiwa baazi ya vifaa.. nime angaika nabima sasa iko tayari kufanya kazi.. Ila akaunt yangu ya bolt hainuruhusu kuwa online.. na kupikea maombi.. naitaji msaada wenu

 6. Nimerequest bolt toka Mombasa ukonga kuelekea bunju A aina ya usafiri bajaji MC121 ya dereva Samsoni kufika bunjuA ikaendelea kuonyesha pande game reserve ambapo sio request yangu akanidai elf 31000 naomba msada wa hili

 7. Mimi Ni abiria Leo nimetoka Chawote kwenda ilala Boma n dereva bodaboda anaitwa komba akafuta safari na bei alivyosema ni tofauti

 8. Bolt mnatutesa madereva wa Arusha location Bado hamjazijua,wateja wanarequest Alafu ukiwa njiani kuwafata wanacancel hiyo asara tunalipwa na nani? Alafu Makato yenu ni makubwa hayana moangilio bei mnaweka ndogo Sana jaman mafuta nighali oil, service ya gari hapo dereva hupati kitu Tajiri anataka esabu yake mnawapendelea wateja kitu ambacho sio kizuri madereva ndio tunaumia Alafu angalieni mteja amerequest unamfata sehemu ya mita 100 au km 1 na ameandika elfu 4 ukifika ndio uanze trip hamuoni tunapata asara kwanini msipigie mara mbili ya Ile Hela ili iwe imefidia kwenda kumfata na kumleta anako kwenda na Makato yenu muweke kwake mfano kumfata imesoma elfu 4 weka elfu name Makato ya elfu nane labla ni elfu Moja miatano wekeni isome Tisa miatano ili dereva apate Ile stahiki yake fanyeni kama TRA wanavyo kata Kodi vat ni ya mnunuzi bolt mnatuumiza sio Siri kama Mimi mmenichukulia Hela ambazo sio sawa na mwanzo nilivyo kua nakatwa

 9. Account yangu iko on but aiingi reguest naukijalbu kuireguest hainisomi kanakwamba inanionesha siko ewani wakati nmeiwasha na iko on

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *