Kama wewe tayari ni dereva au kama ndio unataka kuanza biashara ya Uber au Bolt Tanzania hii makala ni maalumu kwa ajili yako.
Watu wengi huwa wanakosa taarifa sahihi za kuwasaidia kuchagua kampuni ipi wajisajili na kuendesha abiria au ni ipi waikazanie zaidi. Kwa hiyo kwenye makala hii tutaenda kuchambua tofauti za majukwaa haya mawili na jinsi tofauti hizi zinavyoweza kukunufaisha dereva.
IPI ILIANZA? UBER AU BOLT TANZANIA?
Moja ya vigezo vya kufahamu kampuni yenye faida zaidi ni kufahamu ipi ilianza shughuli zake kwenye eneo husika.
Faida za kampuni iliyoanza mapema zaidi
- Huwa ina wateja wengi zaidi kwasababu waliwahi kuanza na kunasa soko.
- Ina uzoefu mkubwa zaidi wa kutoa huduma bora kwasababu imeendeshwa kwa muda mrefu zaidi.
- Ina fedha zaidi za kuweza kushindana na wageni kwasababu imeshafanya vizuri kwenye biashara na ina wawekezaji wengi zaidi.
- Inajitahidi kujiboresha kwasababu inaona makampuni mengi nayo wanaanzisha huduma kama zao hivyo kuleta ushindani mkubwa.
Changamoto za kampuni iliyoanza mapema zaidi
- Wadau wanapokuwa wengi sana ni rahisi kwa ubora wa huduma kushuka.
- Wadau wenye malalamiko au wanaoona wanaonewa huhama kirahisi kwenda kwenye kampuni mpya.
- Kampuni mpya hutumia mapungufu yao kama kigezo cha kuboresha na kutangaza huduma zao hivyo kufanya urahisi wa wadau kuhama.
Sasa tuangalie ni ipi ilianza kabla ya nyenzake:
Uber | Bolt |
Uber ilianzishwa jijini San Fransisco, California mwaka 2009 na hapa Tanzania ilianzisha huduma rasmi mwezi June 2016. | Bolt ilianzishwa nchini Estonia mwaka 2013 na ilizindua kazi zake nchini Tanzania mwaka 2017. |
Kama unavyoona, Uber ilianzishwa kabla ya Bolt. Hii ina maanisha kwamba automatically kampuni ya Bolt iliichunguza Uber na huduma zake, kisha ikachambua mapungufu yake na kuamua kuanzisha kampuni yao na kushindania soko na wabobezi hawa.
Kwa hiyo kimsingi kampuni mpya zaidi huwa zinakuwa na manufaa zaidi kwa wadau kwa muda fulani hadi pale kampuni ya mwanzo inapoamua kubadilika na kujiboresha ili kutompa mshindani nafasi ya kuchukua wateja wake wote.
MAENEO YENYE HUDUMA
Uber | Bolt |
Huduma za usafiri wa Uber zinapatikana Tanzania katika mji mmoja tu ambao ni Dar es salaam. | Bolt Tanzania inapatikana katika miji minne mikubwa ambayo ni Dar es salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza. |
Tathmini: Kampuni ya Bolt ndio inatoa huduma katika maeneo mengi zaidi Tanzania hivyo kuleta fursa kwa Watanzania wengi kuliko kampuni ya Uber.
GHARAMA YA NAULI
Uber | Bolt |
Kutokana na tafiti na taarifa zilizopo, Uber ina bei kubwa ya nauli kuliko Bolt. | Kampuni ya Bolt Tanzania ipo makini zaidi katika kutoza nauli kidogo kuliko Uber. Pia Bolt hutuma promotion za punguzo za bei kwa abiria wake mara kwa mara kuliko Uber. |
Tathmini: Bolt inatoza nauli kidogo zaidi kutokana na sababu tulizojadili hapo mwanzo kuwa kampuni iliyochelewa kuanza huwa inabidi kushindana na iliyo wahi hasa katika bei.
Pia punguzo hili la nauli halimaanishi kuwa linawapunguzia kipato madereva, wote wanafaidika na hili, abiria na madereva.
ADHABU YA KU CANCEL SAFARI NI KUBWA KWENYE UBER AU BOLT?
Uber | Bolt |
Abiria aki cancel safari dakika 2-5 baada ya dereva kuchukua ile safari basi dereva analipwa fidia kiasi. Abiria asipofika kwenye eneo la kuchukuliwa (pick up location) ndani ya dakika 5 ya dereva kuwasili, dereva anapata sehemu ya adhabu ya kuchelewa atakayolipishwa abiria. | Abiria aki cancel safari zaidi ya dakika 2 baada ya dereva kukubali safari atatozwa faini ambayo dereva atafidiwa. Abiria asipofika kwenye eneo la kuchukuliwa(pick up location) ndani ya dakika 4-8 ya dereva kuwasili, dereva anapata sehemu ya adhabu ya kuchelewa atakayolipishwa abiria. |
Tathmini: Uber inatoa faini pale abiria anapo cancel au kuchelewa na wapo serious dakika zikipita tu, faida kwa dereva. Bolt kutokana na ripoti na uchunguzi wa mtandaoni wanaonekana kuwa wepesi zaidi kutowapa faini abiria. Hilo dirisha la dakika 4-8 linatumika vibaya. Mara nyingi abiria huchelewa au hu cancel bila dereva kupata fidia.
IPI INA MAKATO ZAIDI KWA MADEREVA, UBER AU BOLT?
Uber | Bolt |
Uber inachukua kati ya 20% hadi 30% ya nauli yote inayolipwa kwa kila safari dereva anayofanya. | Bolt inachukua kati ya 15% hadi 20% ya nauli anayolipwa dereva baada ya kila safari aliyokamilisha. |
Tathmini: Kampuni ya Uber inachukua kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuliko kampuni ya Bolt.
IPI INALIPA ZAIDI KWA MADEREVA?
Uber | Bolt |
Madereva wa Uber wanapata 79% hadi 80% ya nauli abiia anayolipa. | Madereva wa Bolt wanapata 80% hadi 85% ya nauli kamili. |
Tathmini: Kwa haraka unaweza kusema madereva wa Bolt Tanzania wanapata fedha nyingi zaidi. Lakini kumbuka kuwa nauli za Bolt ni ndogo kuliko za Uber na pia Uber wana wateja wengi zaidi. Hii inaweza kufanya mwisho wa siku faida iwe sawa tu au itofautiane kidogo sana.
USALAMA ZAIDI UPO WAPI?
Uber ina njia nyingi za kuhakikisha usalama wa dereva na abiria ambazo zimeundwa ndani ya app. Moja wapo ni uwezo wa kutrack safari nzima na kuwashirikisha watu wako wa karibu ili wajue ulipo muda wote.
Pia kuna kipengele cha usalama ndani ya app ambacho kinaweza kukuunganisha moja kwa moja na huduma ya usalama 24/7.
Uber pia ina system ya kutoa alama kwa madereva pamoja na abiria ili kusaidia wote wawe wastaarabu na wasimletee mwengine shida.
Safari zote za uber zinafatiliwa na kurekodiwa kwa teknolojia ya GPS kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho kwa hiyo abiria anakuwa na amani kwasababu na yeye anaona kwenye app yake kama kweli anapoelekea ndio anapotaka kwenda.
Kwenye app ya Uber dereva anaweza kuhakiki kama abiria anayemchukua ndio mwenye profile iliyoomba usafiri kwa kutumia PIN.
Bolt pia wana system nzuri ya kuhakikisha usalama kama vile kuweza kutrack safari nzima na kushirikisha watu wako wa karibu wajue dereva au abiria alipo muda wote.
Tathmini: Hatua za usalama zipo vizuri kwa madereva na abiria wote wa Uber au Bolt Tanzania. Pia kampuni zote zina bima inayolinda dereva na abiria wake pale panapotokea ajali.
SOMA: Bima ya ajali ya Uber kutoka Britam
UPOTEAJI WA MALI
Uber | Bolt |
Abiria akisahau kitu kwenye gari anaweza kuwasiliana na dereva ili apelekewe mali yake. Uber itamchaji abiria kiasi sahihi na kumfidia dereva kwa huduma ya kumpelekea mzigo. | Abiria akisahau mzigo kwenye gari, Bolt inamhamasisha kuthamini muda na bidii za dereva kumpelekea mzigo wake na kumlipa ipasavyo. Hakuna kiasi maalumu, abiria anakubaliana na dereva. |
Tathmini: Uber inatoza kiasi maalumu kulingana na safari ya dereva kurudisha mzigo uliosahaulika. Bolt haifanyi hivi, badala yake inampa abiria uwezo wa kuchagua amlipe kiasi gani kwa kumletea mzigo wake.
Hii inaweza kuwa nzuri kwa madereva kwasababu wanaweza kufidiwa kiasi kikubwa zaidi. Lakini pia inaweza kuwa mbaya kwasababu abiria wanaweza kusema hawana fedha hivyo kuwalipa kidogo.
PROMOTION KWA MADEREVA
Uber | Bolt |
Ongezeko la bei maeneo yenye abiria wengi kuliko madereva (Surge pricing) Bonus za kuendesha safari za kufatana yaani ukimaliza moja ukaanza nyingine papo hapo (consecutive trips promo). Punguzo za bei za matengenezo ya gari ( Jerry Spare Parts) | Bonus mbali mbali kila mwezi kwa ajili ya madereva ambao wapo active zaidi na si wale ambao wanakuwa hawafanyi kazi mara kwa mara.. Bima ya ajali kwa ajili ya dereva na abiria. |
Tathmini: Kampuni zote zinajitahidi sana katika kutoa bonus mbali mbali ili kusaidia madereva kupata kipato zaidi.
MTAZAMO WA ABIRIA
Kama unavyofahamu kampuni inayopendwa zaidi na wateja ndio huwa na faida zaidi. Hapa Weibak tunajikita katika kuchunguza mtazamo wa abiria kuhusiana na huduma zinazotolewa na makampuni ya usafiri wa ride hailing kama Uber au Bolt na mengineyo.
Huku mitandaoni kuna majadiliano, machapisho na commenti nyingi sana kutoka kwa abiria juu ya jinsi walivyopata huduma kwenye Uber au Bolt.
Uber | Bolt |
Nauli ni kubwa zaidi lakini huduma inaridhisha. Madereva wengi ni professional na wana huduma nzuri. | Nauli ni ndogo lakini huduma hairidhishi. Madereva wengi sio wastaarabu na wapo wanaofikia hatua ya kupiga, kutishia au kulazimisha abiria walipe kwa njia ambazo abiria hawataki. |
Tathmini: Kwasababu Bolt iliamua kutoa huduma kwa bei ndogo ili kuvutia soko, ubora wa utoaji huduma umepata pigo kubwa. Abiria wengi wanasimulia mtandaoni jinsi ambavyo wamewahi kupata madereva wasiofaa kabisa.
Pia wengi wanasema ni bora walipe nauli kubwa na kupata huduma nzuri kuliko kulipa nauli ndogo na kujiweka kwenye hatari ya kupata huduma isiyokidhi viwango.
Inaonekana suala la ipi ni bora kati ya Uber au Bolt Tanzania linategemeana na mahitaji na mtazamo wa mtu binafsi. Kupitia makala hii tunatumaini umeweza kupata mwanga mpya ambao utakusaidia katika shughuli yako ya kusafirisha abiria kwenye majukwaa haya.
Kama unaendesha abiria Bolt tushirikishe kwenye comments kama umewahi kusikia abiria wakilalamika kuhusu madereva wa Bolt.
Na kama unaendesha Uber, je malipo unayopata baada ya makato yao unaona ni sahihi?
Nitaenda offisinikwao uber/bolt nikajitidhishe kwaichi nilichokisoma apa mtandaoni na asantesana ni.epata uwelewamkubwa sana
Karibu sana Bruno, ni furaha yetu kama umepata uelewa fulani kutoka kwenye makala hii. Karibu sana na endelea kusoma makala zetu ili upate uelewa zaidi.
Katika TAX mitandao UBER nimiongoni mwa kampuni bora kuliko makampuni yote yanayo fanya kazi hizi za TAX mtandao kwa sababu wateja awaangalii bei swala la bei ni lamwisho kabisa kwa wateja wateja wanajali na kuzingatia ni (Muda,huduma bora yaani uhakika wa safari kupatikana gari,na usarama bora wake na mizigo yake,ndio inakuja bei bado bei ni affordable ) sasa UBER hivyo vyote wanavitoa katika huduma zao mpaka kurejesha mali ya mteja iliopotea katika trip
Mfano harisi uliotokea kwangu nikiwa na trip mteja nilisha tapika kwenye gari langu akiwa kalewa mm nika piga picha na kuripoti UBER wakaniuliza Car wash kusafisha ni Tsh ngapi? Nikawajibu wakaniambia nikaoshe zen wakaniwekea pesa next Monday kunirejeshea kwa huduma hii mpaka sasa hakuna kampuny ya TAX mtandao inayo weza toa huduma kama UBER pia 20%-25% sio kubwa kwa dereva kulingana na kazi kubwa ya kutafutiwa wateja cha msingi ninacho kiona hapo ni madereva kuwa na money disprine ( matumizi sahihi ya pesa) maana pesa tunazo zipata ni 3000,4000,5000,6000,7000,8000 nk nindogo sana kama hautajibana kuzitumia kila kitu kikikupita mbele yako unakitaka kamwe pasa haiwezi tosha…! Ila izo pesa ni nyingi sana kama utajiwekea taratibu nzr ya matumizi ya pesa na ujitume kufanya kazi sio muda mwingi unakuwa OFFLINE..
km utatumia ni petrol na chakula au kulipa deni kwenye App na MB tu ikifika muda wa kufunga kazi ukiangalia pesa zako nipesa nyingi mno
Kwakweli bolt kwa madereva inatuumiza sana bei zao hazilizishi ata kidogo
habari, naitwa selemani sharaha nina tatzo akaunti yangu haipokei request ni siku ya4 sasa tangu nilipe deni naomba msaada wenu.