tengeneza kipato kwa kuendesha uber tanzania

TENGENEZA PESA KWENYE UBER KWA KUSAIDIA MADEREVA WAPYA KUANZA

Madereva wengi hawafahamu kuwa zipo zaidi ya njia moja ya kutengeneza pesa nyingi kupitia jukwaa la Uber. Kwenye makala hii utaenda kuona jinsi ya kutengeneza pesa kwenye Uber kwa kupitia programu ya Uber referral.

Kama ambavyo tumeandika mara nyingi kwenye makala zetu, kampuni ya Uber inaongoza katika sekta hii ya usafiri kwa kutumia programu. Hii inamaanisha kuwa kampuni inahitaji madereva wengi ili abiria wasikose au kuchelewa kupata huduma.

Kutokana na uhitaji wa abiria Uber ilianzisha fursa nzuri sana kwa madereva na abiria kutengeneza pesa ya ziada kwa kuleta madereva wengine au abiria wengine kwenye jukwaa.

Katika makala hii tutaenda kuongelea jinsi ya kutengeneza pesa kwa kuingiza madereva wengine kwenye Uber.

TENGENEZA PESA KWENYE UBER KWA KUSAJILI MADEREVA WAPYA

Dereva yoyote anayeendesha Uber anaweza kutengeneza fedha kwa njia hii kwa kupitia hatua 3

  • ALIKA: Tuma mwaliko kwa marafiki, ndugu au wafuasi wako wajumuike na wewe katika kutengeneza pesa kwa kuwa madereva Uber. Mwaliko huu utaambatanishwa na code ambayo ipo kwenye dashboard yako ya app ya dereva.
  • FATILIA: Watu wote watakaoitikia mwaliko wako na wakatumia referral code yako kujisajili kuwa madereva wataorodheshwa kwenye dashboard ya application yako ya dereva. Kwa hiyo utajua kama wameshakubaliwa na watakapoanza kukubali safari.
  • PATA MALIPO: Baada ya watu wako waliojisajili kupitia referral code yako wakimaliza safari kadhaa utaona malipo yako kupitia dashboard ya app yako ya dereva.

REFERRAL CODE UNAIPATA WAPI?

Ili kupata code ya kuwatumia watu, ingia kwenye app na ubonyeze ” Earnings” (mapato). Chini kabisa ya screen utaona kipengele cha “Invite Friends Now”, bonyeza na utapata code yako chini kabisa kwenye screeen tayari kwa kuisambaza.

Katika kipengele hiki pia ndio utakapokuta watu wako wote waliojisajili na code yako. Utaweza kuona maendeleo yao na watakapotimiza safari zinazotakiwa kwa wewe kupata kipato.

Kwa kutumia compyuta unaweza kupata referral code yako kwa kutembelea partners.uber.com ingia kwa kutumia email au namba ya simu pamoja na password uliyotumia kujisajili kama dereva.

Kisha tafuta kipengele cha “Invites” ili kupata code na kuona maendeleo ya watu waliojiunga kwa kutumia code yako.

Pale dereva mpya atakapoingiza referral code yako wakati anajiandikisha kuwa dereva wewe utatumiwa email kwenye account uliyotumia kujisajilia Uber.

KIASI GANI CHA FEDHA UTALIPWA

Zamani dereva alikuwa analipwa kiasi cha 50,000/= tsh kwa kila dereva aliyejiunga Uber kwa kutumia referral code yake.

Sharti lilikuwa kwamba hela hii unapewa baada ya huyo dereva kumaliza safari 20 kwenye jukwaa hili. Hii ilikuwa inachukua muda mrefu sana kwa hiyo Uber ikaamua kuongeza motisha na kupunguza masharti.

Kwa sasa dereva anaweza kupata 100,000/= tsh kwa kila dereva mpya atakayejisajili kwa referral code yake na atakapokamilisha safari 5 tu.

PESA HUINGIA KWENYE AKAUNTI YA DEREVA BAADA YA MUDA GANI?

Baada ya dereva mpya kumaliza tripu 5, Uber itaanza kushughulikia malipo yako wewe mwenye referral code. Baada ya wiki mbili hela zitaingizwa kwenye akaunti yako. Taarifa za malipo utazikuta kwenye app ya dereva katika kipengele cha “Miscellaneous or other payments”

Dereva pia unaweza kupata kiasi kidogo kwa kutoa code kwa ajili ya abiria wapya kama hivi kwa madereva wapya. Lakini ya madereva ndio ina malipo makubwa sana na faida zaidi.

JINSI YA KUPATA MADEREVA WA KUWAPA CODE YAKO

Kama ambavyo umeona, programu hii inafaida kubwa sana na inaweza kuzidisha jumla ya kipato chako kufikia mamilioni ndani ya muda mfupi tu!

Cha muhimu ni kuwekeza muda mchache wakati hauna abiria wa kusafirisha ili kutafuta watu wanaotamani kujiunga na Uber. Unaweza kupata watu wengi kwa kufata njia zifuatazo

1. TUMA UJUMBE MFUPI (SMS) KWA CONTACT ZAKO

Tumia app yako ya dereva kutuma mualiko wa udereva kwa watu wako wote uliowahifadhi kwenye simu yako (contact list). Lipo chaguo la kutuma ujumbe moja kwa moja kutoka kwenye app yako kwenda kwa contact list yako. Cha kufanya ni kuongeza tu ujumbe wako wa kushawishi na kisha kutuma kwa watu wote.

Watu wengi siku hizi hupendelea kutumia whatsapp kuliko sms kwasababu ni rahisi zaidi kutuma picha, video, documents na links.

Chukua link yenye referral code yako kupitia app yako ya dereva kwenye simu au kwenye computer kisha uisambaze kwa broadcasting, whatsapp status au kwa kumtumia mtu mmoja mmoja.

3. TUMA KWENYE MITANDAO YA JAMII

Watu wengi sana wana kurasa za mitandao ya jami na wana wafuasi wengi ambao wanaweza kuwatumia kama chanzo cha kipato.

Badala ya kutumia mitandao hii kama chombo cha kupoteza muda tu, geuza wafuasi wako kuwa kipato kwa kuongelea kuhusu faida za Uber na kuwatumia referral code yako wajiunge.

Unaweza kutuma pia kwenye magroup yako ya facebook maana huko kuna watu wengi zaidi na hivyo hautakosa madereva wanaotaka kujiunga.

4. ANZISHA GROUP LA FACEBOOK

Kama tayari una ukurasa wa facebook ni rahisi sana kuanzisha group na kuanza kuelimisha kuhusu jinsi ya kuanza biashara ya Uber.

Wapo watu wengi sana ambao wanahitaji ajira lakini hawajui pa kuanzia. Elimu yako itawafikia wengi watajiunga na itakuwa rahisi kuwapa referral code yako na kutengeneza pesa ya ziada.

5. ANZISHA HUDUMA YA KUSAJILI MADEREVA

Sio kila mtu anaweza kuingia kwenye mtandaoni, kutafuta tovuti ya Uber na kujiandikisha. Wapo wengi wenye vigezo lakini wanakwama katika hatua hii ya kwanza.

Ili kuhakikisha unapata pesa nyingi zaidi jitangaze kuwa unasaidia madereva kujisajili. Waelekeze kuhusu nyaraka zote wanazozihitaji, wakishamaliza kuzikusanya, kutana nao na uwaongoze katika kujaza fomu za mtandaoni.

Itakapofika sehemu ya kuweka referral code weka ya kwako na uwaelekeze kwanini unaiweka. Kisha utakuwa umepanda mbegu ambayo baadaye utakuja kuvuna 100,000/= tsh kwa kila dereva.

Hii ndio njia bora zaidi kwasababu utahakikisha kila dereva anaingiza code yako wewe na hakuna mwingine anayeweza kuwapa code yake. Pia unaweza kuwasaidia kuwasajili bure au kwa ada ndogo tu ya muda ule na wakaridhika pia.

5. FUNGUA CHANNEL YA YOUTUBE

Hii ni fursa nzuri sana ambayo sio madereva wengi wanaichangamkia. Unaweza kupata madereva wengi wa kuwasajili na referral code yako kwa kutengeneza video za kuelimisha na kuburudisha youtube.

Watu wengi wanapenda kujifunza kwa kuona hivyo itasaidia kushawishi zaidi wakutafute uwasaidie kujisajili.

Hakikisha unasema dhahiri kuwa wakutafute watu wanaotaka kuanza tu. Wakikutafuta ambao tayari wameshajisajili itakupotezea muda maana hautaweza kujibu kila mtu maswali bure.

Ama unaweza kukubali kujibu watu maswali kwa undani zaidi kwa kuwachaji kiasi fulani kuwaelimisha.

Uzuri wa youtube pia utaweza kupata fedha kutoka kwa youtube pale utakapofikisha wafuasi 1000 na video zako zitakapoangaliwa kwa masaa 4,000.

6. ANZISHA BLOG

Kama hauwezi kutengeneza video za kuelimisha basi unaweza kuandika makala za kuelimisha katika blog yako. Hii pia itakuletea madereva wapya wengi maana utakuwa unawapa elimu ya bure kwa kuandika makala kama:

Jinsi ya kujisajili kuwa dereva Uber na kukubaliwa haraka 2022

Jinsi ya kujiajiri na kutengeneza pesa nyingi kupitia Uber

Tunatumaini umepata kitu kupitia makala hii. Tafadhali share makala hii na madereva wengine ili nao waweze kuona jinsi ya kutengeneza pesa Uber kwa kusaidia madereva wapya kujiunga.

Kama umewahi kutumia mbinu hii ya kutengeneza pesa kwenye Uber tafadhali tushirikishe experience yako ili tujifunze zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *