Jinsi Sakata la Uber, Bolt lilivyowaathiri Wamiliki wa Magari
Ni kwa namna gani kusitishwa kwa huduma kwenye majukwaa ya Uber na Bolt kumeyaathiri maisha ya wamiliki wa magari?
Ni kwa namna gani kusitishwa kwa huduma kwenye majukwaa ya Uber na Bolt kumeyaathiri maisha ya wamiliki wa magari?
Wakati Uber imesitisha huduma zake nchini, na Bolt kusitisha huduma za usafiri wa gari kwa abiria binafsi, abiria pamoja na madereva wanajaribu kutumia majukwaa mengine ili kupata huduma ambazo wamezikosa kutokana na changamoto walizonazo Uber na Bolt.
Agosti 17,2022, Bolt ilisitisha huduma zake za magari kwa abiria wa kawaida na kujikita zaidi katika abiria wa makampuni. Hali hii ikiwa imekuja miezi minne tu, toka Uber isitishe baadhi ya huduma zake Tanzania, wote wakilalmikia viwango vipya vya nauli na kamisheni vilivyopitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Haya ni matukio muhimu kwenye sakata hili:
Watu wengi wametambua na kuanza fursa ya kutengeneza mamilioni kwa kuendesha abiria kwenye majukwaa ya safari kama Uber na Bolt. Lakini je? Ni kila mtu anaweza kutengeneza kipato cha kutosha kwa njia hii? Madereva wengi hasa wale wapya huanza kazi hii bila kujifunza misingi muhimu zaidi ya kuwafanya wafanikiwe. Kama wewe ni dereva au mmiliki …
JINSI YA KUTENGENEZA PESA NYINGI KWENYE UBER/BOLT Read More »