Sheria za utoaji huduma Uber/Bolt

SHERIA ZA UTOAJI HUDUMA KWENYE JUKWAA LA UBER/BOLT

Kampuni zote zinayofanya shughuli za biashara lazima ziwe na sheria za utoaji huduma ili kuhakikisha wateja wao wanaridhika na kurudi tena na tena.

Unapoendesha abiria kwenye majukwaa haya ya Ride-sharing/Ride-hailing wewe unakuwa unawasilisha picha ya kampuni kwa abiria. Kutokana na hili kampuni hizi zinataka utoe huduma kwa kufata kanuni zifuatazo.

1. Uhakiki wa abiria.

Dereva wa Uber au Bolt analo jukumu la kuhakikisha kuwa anamchukua abiria sahihi aliyeitisha usafiri. Zipo shuhuda nyingi tu ambazo madereva wamebeba abiria ambao sio na hivyo mwisho wa siku kupata lawama na kupoteza kipato cha safari hizo.

Sheria za utoaji huduma Uber/Bolt

Hakikisha unamuuliza abiria wako jina na mahali anapoelekea ili kuepuka usumbufu huu.

2. Heshima na ustaarabu

Madereva wanatakiwa angalau kuwasalimia abiria kabla ya kuanza safari ili kujenga mahusiano mazuri. Customer care ni muhimu sana kwasababu itakufanya kupata alama(ratings) nzuri zaidi. Pia itakuwezesha kuweza kupata fursa nyingine ya mahusiano zaidi na abiria kwasababu tu ya kupendezwa na huduma yako.

3. Lugha na mazungumzo sahihi

Siku zote dereva anatakiwa kuwa na busara katika mazungumzo na abiria wake. Hautakiwi kuwaongelesha abiria kwa ukali wala kwa kutumia maneno ya matusi au vitisho.

Hautakiwi pia kuanzisha mazungumzo ya undani sana , ya kimapenzi au kingono. Umakini mkubwa unatakiwa kuzingatiwa katika kuwasifia abiria wako hasa wa jinsia tofauti. Usitoe sifa za kimaumbile kama kusifia shape, makalio, maziwa nk.

Mahusiano yako na abiria yanatakiwa kuwa ya kikazi zaidi maana wewe ni kama muwakilishi wa kampuni ya Uber/Bolt kwao. Ustaarabu wako na mazungumzo mazuri yanaweza kufanya mtu ajisikie vizuri sana, hasa kwasababu watu wana mambo mengi yanayowasumbua kichwani.

4. Kugusana

Hakuna ulazima wa dereva na abiria kugusana kwa lolote lile. Ni vizuri kuepuka kugusanana na watu usiowafahamu kwasababu watu wengi hawapendelei hili. Pia wengine imani zao hairuhusu kabisa kugusana na watu hasa wa jinsia tofauti.

Hii pia inasaidia kupunguza malalamiko hasa kama hauna Camera kwenye gari lako. Wakati ambao unaweza kuwa sahihi kugusana na abiria wako ni pale anapokuwa anahitaji msaada wa kuingia au kushuka kama anatatizo la kiafya.

4. Unyanyasaji wa kijinsia

Kanuni za madereva Uber na Bolt Tanzania

Kuna aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia na hizi zote hautakiwi kabisa kuzifanya. Epuka tabia zifuatazo ili kuhakikisha hauvuki mipaka ya mtu.

  • Epuka kuuliza abiria wako kama wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi au la, au kama wameolewa au kuoa nk
  • Epuka kutoa sifa za kimapenzi kwa abiria wako. Mfano ni kusifia maumbile yao kama makalio, kifua au shape ya mwili.
  • Epuka kuongea lugha au maneno ya kimapenzi.
  • Usimtamanishe abiria wako kimapenzi yaani ku -flirt kwa maneno, ishara au kuwagusa.
  • Usioneshe abiria wako picha, video au hata sauti zenye maudhui ya kingono.
  • Hairuhusiwi kufanya mapenzi na abiria wako hata kama muwe mnafahamiana au la.

5. Ubaguzi

Mfano mwengine wa sheria za utoaji huduma ni kutobagua abiria kwa njia yoyote ile. Katika biashara kila mteja ni sawa na wanapaswa kuhudumiwa kwa usawa. Mfano wa aina za ubaguzi ni ule wa rangi, wa asilia, jinsia, umri, ulemavu, dini na hata ubaguzi wa eneo ambalo abiria wanaelekea au kutokea.

6. Helmet na mikanda

Ni lazima kila dereva ahakikishe abiria wake wanachukua hatua za usalama barabarani ili kuhakikisha usalama wao wakati wa dharura. Abiria wote wa pikipiki (Boda boda) lazima wavae helmet inayowatosha vizuri. Na abiria wa magari wafunge mikanda hata kama wamekaa siti ya nyuma.

7. Heshima kwa sheria za barabarani

Usalama wa abiria upo mikononi mwa madereva, hivyo makampuni ya usafiri hutaka wateja wao wamalize safari wakiwa salama kama walivyoanza safari. Unapaswa kuzingatia sheria na kanuni zote za barabarani ili kuhakikisha unatengeneza pesa nzuri kwa huduma yako.

Kwa mfano hauruhusiwi kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu umakini wa kuendesha gari kama kushikilia simu mkononi mwako wakati gari linakwenda. Pia hauruhusiwi kuendesha kwa kasi ya kuzidi kimo cha barabara husika au kuleta fujo na kugombana na madereva wengine.

8. Utapeli

Hairuhusiwi kufanya mbinu zozote za kufanya abiria wako alipe gharama kubwa kuliko urefu wa safari yake. Hii inajumuisha kupita barabara tofauti yenye umbali mrefu zaidi ya ile iliyokubaliwa na abiria. Kufanya GPS isome safari kimakosa ili kukufaidisha wewe.

Pia hairuhusiwi kusimama hovyo wakati wa safari bila ruhusa ya abiria wako. Pia abiria anapolipia safari yake, hauruhusiwi kuchukua abiria mwengine aidha kwenye jukwaa jingine au tu abiria wako binafsi.

9. Nyaraka halali

Dereva ni lazima uwe na leseni zote (ikiwa ni pamoja na leseni halali ya dereva), vibali, bima ya gari, bima ya gari, usajili, vyeti na hati nyingine.

Pia unatakiwa kuwa na vifaa vya usalama kama helmet, na jaketi la usalama pamoja na vifaa vingine vya usalama vinavyohitajika na mamlaka husika katika kutoa Huduma za Usafiri.

10. Kugawa akaunti

Hairuhusiwi kwa dereva kumpa akaunti yake mtu mwingine ambaye hajasajiliwa. Hii hutokea mara nyingi sana na abiria wengi hulalamika kuwa wamefatwa mara nyingi na madereva ambao sura zao hazifanani na picha ya kwenye akaunti zao.

Akaunti za madereva wanaoruhusu madereva wasiosajiliwa kuendesha abiria kwa niaba yao hufungwa mara wanapobainika.

SOMA HAPA kufahamu vigezo vya kukubaliwa kuendesha abiria wa Bolt.

Nini hutokea ukuvunja sheria za utoaji huduma?

Majukwaa ya usafiri hasa Uber na Bolt ni marahisi sana kusimamisha akaunti ya dereva pale anapovunja sheria za huduma. Na ubaya ni kwamba kupata muhudumu wa customer care wa kutatua jambo hili ni mtihani mkubwa .

Fahamu jinsi ya kuwasiliana na mtu wa huduma kwa wateja (Customer care) wa Uber unapokuwa na malalamiko.

Hakikisha hauvunji sheria hizi ili uweze kuendesha kwa amani na kutengeneza fedha nyingi zaidi. Ni vizuri pia kama utaweza kutembelea tovuti za majukwaa haya ya usafiri ili kujifunza mengi zaidi kuhusu sheria za kutoa huduma.

Kama wewe ni dereva wa Bolt pitia hii makala ya vigezo vya kutoa huduma kwa wateja au abiria wa Bolt. Kwa madereva wa Uber unaweza kupata hapa makala ya sheria za utoaji huduma kwa wateja wa kampuni hii.

Kama wewe ni dereva wa Uber pitia hapa kusoma zaidi kanuni za utoaji huduma kwa madereva wa jukwaa hili. Makala yake yake haijatafsiriwa kwa Kiswahili kwa hiyo ni bora zaidi kusoma tu makala yetu kwasababu inaelezea vitu ambavyo vipo kule.

Usisahau kujisajili kwenye website yetu ya Weibak Carsharing ili uweze kupata dondoo zote kuhusu jinsi ya kufanikiwa sana katika biashara ya kuendesha abiria kwenye majukwaa kama Uber na Bolt.

Kila wiki tunachapisha makala mpya za kuelimisha ambazo zitakusaidia kuzidisha kipato chako maradufu!

Tutafurahi sana kama utaweza kushare makala hii na madereva wengine au wamiliki magari ili na wao waweze kupata maarifa ya ziada.

Je, kuna sheria yoyote tumeiruka? Tafadhali tushirikishe kwenye sehemu ya komenti hapo chini.

2 thoughts on “SHERIA ZA UTOAJI HUDUMA KWENYE JUKWAA LA UBER/BOLT”

  1. Pingback: SABABU ZA KUFUNGIWA AKAUNTI YA DEREVA UBER

  2. Nimefungiwa akaunt kwasababu vibali vimeisha lakin nimepambana nimepata vibali napikiki nimebadilisha nakuweka piki piki nyingine navibali vingine lakin naona kimya mpka mda huu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *