Uber au Bolt ipo bora tanzania 2022

Sakata la Uber na Bolt: Mfululizo wa Matukio Muhimu

Agosti 17,2022, Bolt ilisitisha huduma zake za magari kwa abiria wa kawaida na kujikita zaidi katika abiria wa makampuni. Hali hii ikiwa imekuja miezi minne tu, toka Uber isitishe baadhi ya huduma zake Tanzania, wote wakilalmikia viwango vipya vya nauli na kamisheni vilivyopitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Haya ni matukio muhimu kwenye sakata hili:

Disemba 21, 2021

LATRA inaitisha kikao cha wadau wa taksi za mtandaoni kujadili nauli pendekezwa za huduma za taksi za mtandao.

Machi 14, 2022

LATRA inatoa muongozo wa mabadiliko ya nauli ambako nauli ya chini kwa safari inafanywa kuwa Sh.3,000 na kiwango cha juu cha kamisheni kwa wamiliki wa majukwaa ya taksi mtandaoni kinawekwa kuwa 15%.

April 8, 2022

Viwango vipya vinaanza rasmi kufanya kazi. Baada ya hapo LATRA inawaandikia amri ya utekelezaji baadhi ya wamiliki taksi-mtandao ambao hawakufuata viwango vipya, hii ni hatua ya kwanza Mamlaka huchukua ikielekea kutoa adhabu kama kusimamisha au kufuta leseni.

April 12, 2022

Madereva wa taksi  mtandao wanaandamana mpaka ofisi za  LATRA wakitaka wamiliki wa mifumo ya mtandaoni hasa Uber kuwajibishwa kwa kushindwa kuweka viwango vipya kwenye mifumo yao

April 14, 2022

Uber inatoa taarifa kuwa inasitisha huduma zake za magari Tanzania na kuelezea kuwa kanuni zilizopo zimefanya biashara kuwa ngumu kwa upande wao. Baadae walipeleka lalamiko Baraza la Ushindani, hata hivyo walikuja kuliondoa

Julai 9, 2022

Rais Samia anamteua Habibu Suluo kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa LATRA

Agosti 16, 2022

Bolt inatangaza kuwa kuanzia Agosti 17,2022, magari katika jukwaa lake yatapatikana kwa wateja wa makampuni na kuelezea kuwa mazungumzo na LATRA yamechukua muda mrefu na hivyo kuhatarisha uhai wa biashara ya Bolt Tanzania

Agosti 16, 2022

LATRA inatoa taarifa kupokea taarifa ya Bolt na kuwataka abiria kuendelea kutumia huduma zingine za taksi mtandao ikiwemo Littleride, Ping na Paisha

Agosti 19, 2022

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA anasema bado wanataka Bolt na Uber ziendelee kufanya kazi nchini na “anaamini katika mazungumzo changamoto hizo zitamalizika”. Anawakaribisha kwa mazungumzo.

Agosti 20, 2022

Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva Mtandaoni, Fredy Peter, anaisihi serikali isiruhusu kuweka kamisheni zaidi ya iliyopo na kusema kama Uber na Bolt wameshindwa kufuata sheria waondoke wawaachie wengine.

Septemba 5 na 8, 2022

LATRA inafanya vikao na Chama cha Madereva wa Teksi Mtandao Tanzania (TODA), kampuni za Bolt na Uber ili kusaidia utoaji wa huduma bora na endelevu za usafiri kwa kujali maslahi ya mmiliki wa mfumo, wasafirishaji na abiria.

Septemba 12, 2022

Kupitia mitandao ya kijamii, LATRA inatoa taarifa za kufanyika kwa vikao hivyo, ikisema kuwa mazungumzo hayo yalikwenda vizuri na kwamba inasubiri kukamilika kwa baadhi ya taratibu za kimaandishi kabla haijatangaza maamuzi yaliyofikiwa na mamlaka hiyo.

2 thoughts on “Sakata la Uber na Bolt: Mfululizo wa Matukio Muhimu”

    1. Athuman ni Kweli huduma bado hazijarudi na sababu kubwa ni kwamba kampuni husika bado zipo katika mazungumzo na mamlaka (LATRA). Tutaendelea kutoa updates ya kila kitakacho endelea kutokana na mazungumzo hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *