PROMOTION ZA UBER QUEST

PROMOTION ZA UBER QUEST: TENGENEZA PESA ZAIDI!

Kwa madereva wa Uber promotion za Uber Quest inaweza kusaidia mapato yako kupanda hadi kiwango cha juu ndani ya muda mchache.

Wakati mwingine kipato kwenye jukwaa la Uber huwa chini sana ingawa kampuni hii wanalipa vizuri kidogo ukilinganisha na kampuni nyingine. Kwa hiyo ni muhimu wewe kama dereva kutumia kila fursa ambayo kampuni imeweka ili kukusaidia kuongeza faida kwenye biashara ya Uber.

SOMA: Jinsi ya kutengeneza fedha ningi zaidi Uber

PROMOTION ZA UBER QUEST NI NINI?

Madereva Uber wengi hawafahamu jinsi promotion za Uber Quest zilivyo na jinsi zinavyoweza kuwanufaisha.

Ndio maana sisi hapa Weibak Carsharing tumejikita katika kutoa elimu makini kabisa ili kuhakikisha madereva wote wananufaika sana kama wanavyonufaika madereva wa kwenye nchi za nje ambapo majukwaa haya yametokea.

Ukweli ni kwamba usipojikita kujifunza mbinu kabambe hasa ambazo tumezichambua kwenye blog yetu basi utakuwa unakosa nafasi ya kuongeza kipato kikubwa sana!. Kwahiyo ni vizuri kama utaweza kutenga muda kidogo kwa siku kupitia makala na kujifunza mapya.

Sasa twende kwenye Uber quest!: Hizi ni promotion ambazo Uber hutoa bonus kwa madereva baada ya kufikia malengo ya kukamilisha idadi fulani ya safari ndani ya muda fulani.

Promotion hizi mara nyingi hutokea kama tangazo linalosema “Pata tsh kiasi fulani kwa kukamilisha safari 10 kuanzia saa hii mpaka saa hii”

Dereva unaweza kuona promotion ya Uber quest kwenye app yako ya dereva kwa kupitia kipengele chaPromotions“. Huko utaona quests zilizopo na utaweza kuchagua ipi unaona kama utaweza kuimudu.

Aina 2 za zawadi za promotion za Uber quest.

  1. FEDHA: Kama tulivyosema hapo mwanzo kuwa dereva anaweza kupata kiasi fulani cha fedha baada ya kumaliza quest yake ya idadi fulani ya safari ndani ya muda ulioelekezwa.
  2. PUNGUZO LA ADA: Uber service fee quest huwa na zawadi ya punguzo la gharama ya uendeshaji biashara Uber. Yaani utakuta promotion inasema “Pata punguzo la 20% kwenye ada yako ya dereva Uber ukimaliza safari _ kuanzia saa_ hadi saa_”.

Jinsi ya kupata Uber service fee quest.

  • Nenda kwenye kipengele cha “Promotions” kwenye app yako ya dereva.
  • Kama kuna promotions zozote utaona zimewekwa. Kisha chagua unayoona ina manufaa makubwa kwako.
  • Kubali quest kwa kubonyeza “Choose this quest”
  • Anza safari ukamilishe quest.

Utakapomaliza zile safari zilizotajwa basi utapata notification kuwa kwa safari zinazofata Uber itakata nauli kidogo zaidi kulingana na zile asilimia za punguzo ulizoshinda.

Zawadi ya punguzo inakuwa milele?

HAPANA: punguzo linakuwa ndani ya ule muda wa quest tu.

Kwa mfano promotion inaweza kusema “Service fee itakuwa 13% (badala ya 20% – 30% ya kawaida ya Uber) kama utaweza kukamilisha safari zaidi ya 7 kuanzia Ijumaa saa kumi alfajiri hadi Jumatatu saa kumi alfajiri”.

Hii inamaanisha kuwa muda wowote ndani ya siku hizi tatu ukikamilisha safari hizi basi kuanzia hapo hadi hiyo jumatatu saa tisa na dakika hamsini na tisa utakuwa unakatwa na Uber 13% tu ya nauli.

Inamaana ukikamilisha safari zako zaidi ya 7 mapema basi utafaidi zaidi punguzo la makato kuliko ukichelewa kufikisha.

Faida za promotion za Uber quest.

Kwanza kabisa ni fedha ya ziada unayopata kwenye quest za kushinda fedha.

Pili punguzo la ada ya Uber ni zuri sana kwasababu tayari watu wengi wanalalamika kuwa Uber wanakata hela nyingi sana.

Tatu ni kwamba hakuna kushindwa, ukamilishe usikamilishe bado unapata faida kwasababu quest imekupa mwamko wa kupata safari nyingi zaidi hivyo kutengeneza kipato kingi zaidi.

Juu ya hayo yote hakuna adhabu wala pungufu lolote au hasara utakayoipata kama utakubali quest na kushindwa kuikamilisha ndani ya muda uliotajwa. Muda wa quest ukishapita unaweza kusubiria kisha kujiunga na quest nyingine na kuanza upya au kuendelea kufaidi zawadi.

DEREVA ANAWEZA KUJIUNGA KWENYE PROMOTION ZA UBER QUEST KWA MKUPUO?

Wakati mwingine unaweza kwenda kwenye kipengele cha promotions na ukakuta quest zaidi ya moja zenye zawadi tofauti.

Kwa mfano unaweza kukuta promotion moja inasema “pata bonus ya tsh 4,000/= kwa kukamilisha safari 2 “. Nyingine inasema “Pata bonus ya tsh 7,000/=kwa kukamilisha safari 5” . Na nyingine “Pata bonus ya tsh 10,000/= unapokamilisha safari 8”.

Ukikamilisha safari 8 haimaanishi kwamba utapata ile zawadi ya safari 2, na ya safari 5 na ya safari 8. Bali utatakiwa uchague quest moja na hiyo ndio utashindia zawadi yake.

PROMOTION ZA UBER QUEST ZINA KIKOMO CHA ZAWADI YA FEDHA?

HAPANA, zipo promotion ndogo za fedha ndogo na pia promotion kubwa zenye zawadi kubwa zaidi na muda mrefu zaidi wa kukamilisha.

Pia app yako ya Uber itakuwa inaweka rekodi ya safari zako ambazo umekamilisha katika quest. Hii ni ili ikusaidie kukupa motisha ya kuongeza bidii ya kufikia lengo na kushinda dawadi.

Unajuaje kama promotion za Uber quest zipo tayari kwa ajili yako?

  • APP YA DEREVA: kwenye kipengele cha Promotions utakuta quests za kuchagua.
  • EMAIL: Unapojisajili Uber utakuwa ulitumia anwani ya barua pepe ambayo hii ndio Uber hutumia kukutumia taarifa mbalimbali kuhusu kampuni kama mabadiliko na promotion kama hizi.

Sio kila dereva anaweza kupata hizi promotion quests. Uber inatumia algorithm yake kutambua madereva wenye alama nzuri, walio active mara nyingi kwenye app (yaani wanaoendesha mara kwa mara) na wenye review nzuri. Hawa ndiyo mara nyingi huwekewa hizi quests kwenye kipengele cha promotion.

Wakati mwingine ni kama bahati tu, unaweza kukuta review zako si nzuri sana na alama za nyota si nzuri kupita wengine lakini bado ukapata quests!. Kwa hiyo usikate tamaa kama hadi sasa bado haujawahi kupata.

Promotion za Uber quest ni nzuri sana kwa ajili ya kutengeneza kipato zaidi kwenye jukwaa hili. Kama bado haujaanza kupata quests zozote endelea kuchunguza kipengele cha promotions kwenye app yako ya dereva.

Pia jenga tabia ya kuangalia inbox ya barua pepe/email yako kila siku ili kuhakikisha haukosi taarifa pale ambapo utakuwa umeunganishwa na huduma ya promotion za Uber quest.

Je, umeshaanza kupata promotions hizi kutoka Uber? Tushirikishe ili madereva wengine nao wahamasike.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *