Mbinu za Kukusaidia Dereva wa Teksi Mtandao Kutengeneza Faida Kwenye Pesa Unayoingiza

Haijalishi hii ni kazi yako pekee au ya ziada, kuendesha gari kupitia majukwaa ya teksi mtandao kama Bolt na Paisha kunaweza kuwa njia nzuri ya kukupatia pesa kwa ratiba yako mwenyewe. Lakini kufanikiwa kama dereva wa teksi mtandao  kunahitaji  zaidi ya leseni na gari.

Tumefanya utafiti kujua namna ambavyo madereva bora wa  teksi mtandao wameweza kufanikiwa kufika kileleni kwa kutengeneza faida kubwa – na jinsi unavyoweza kuwa miongoni mwao. Hizi hapa ni mbinu 8 zinazoweza kukusaidia kutengeza faida zaidi katika pesa unayoingiza kama dereva wa teksi mtandao.

SOMA ZAIDI: Je, dereva unajihisi kunyonywa na majukwaa ya teksi mtandao?

1. Weka gari lako kwenye hali nzuri.

Gari bora zaidi kwa dereva wa teksi mtandao ni lile ambalo halichukui gharama kubwa kufanya matengezo, lisilotumia mafuta mengi na (bila shaka) ambalo ni rahisi kuliendesha. Lakini bila kujali ni aina gani ya gari unaendesha, hakikisha kuwa iko katika hali nzuri – ndani na nje.

Gari lisilotumia mafuta mengi au pesa nyingi kufanya matengenezo litakuepusha kutumia pesa nyingi kuligharamia, badala yake pesa hiyo itakuwa sehemu ya faida uliyoingiza.

2. Hakikisha gari lako lina bima

Ikiwa gari lako lina bima, hutaweza kupata ‘stress’ hasa pale gari lako linapopata ajali. Mfano, kama bima uliyolipia inaruhusu kufanya matengenezo au pengine kubadilishiwa kabisa gari, ni rahisi sana kulifanyia matengenezo bila kutoa pesa yako ambayo umetumia muda mwingi kuitafuta.

Badala ya kutoa pesa yako ya faida uliyoingiza kwa kufanya kazi ndani ya mwezi au mwaka mzima, bima hii zitakusaidia kugharamia matengenezo endapo gari lako litapata ajali.

3. Fuatilia gharama zako

Hakikisha unaweka kumbukumbu ya kila pesa utakayoitumia kwa ajili ya gari lako. Mfano gharama za mafuta, ada za maegesho, malipo ya gari na zaidi. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha fedha umeingiza kwa siku – ukitoa gharama ulizotumia kulihudumia gari lako.

Hii pia itakusaidia kuangalia jinsi ya kupunguza gharama unapolihudumia gari lako ili pesa utakayoingiza ibaki kama faida.

4. Epuka kuendesha gari bila abiria

Usizunguke maeneo mbalimbali kutafuta abiria. Unachofanya ni kukusanya ‘mileage’ na kupoteza mafuta bila kuingiza pesa. Badala yake, egesha gari lako mahali fulani na usubiri ‘requests’ za abiria.

SOMA ZAIDI: JINSI YA KUTENGENEZA PESA NYINGI KWENYE UBER/BOLT

5. Kuwa na ufahamu wa kijiografia wa eneo unalofanyia kazi

Usitegemee sana GPS au Google Map yako. Inaweza kukupotosha. Kujaribu kuyajua na kuyakariri maeneo inaweza kuwa ni njia ya kizamani, lakini inaweza kukusaidia zaidi hasa pale unapopata changamoto za GPS au Google Map. Utakuwa na njia za mkato na njia mbadala iwapo njia unayoitumia itakuwa na foleni, inafanyiwa matengenezo au imefungwa.

Hii itakusaidia kuepuka kupita njia ndefu na kupelekea kutumia mafuta mengi katika safari moja.

Pia, ukishakua na ufahamu wa maeneo yenye abiria wengi wa teksi mtandao, hii itakusaidia sana kujua ni maeneo gani mazuri kwa kusubiri ‘requests’ za abiria.

6. Toa msaada kwa abiria wako

Kutoa msaada zaidi kunaweza kufanya kila safari kudumu kidogo, lakini italipa baada ya muda mrefu. Kwa kawaida, abiria wanapenda kuendeshwa na dereva anayewajali.

Si madereva wote wa teksi mtandao hutumia muda wao kuwasaidia abiria wao na mizigo yao. Kuchukua hatua hii ya ziada kunaweza kukusaidia kuwa tofauti. Hii sio tu itakusaidia kupata nyota tano kwenye ratings, bali itakusaidia kujenga mahusiano mazuri na abiria wako, na kuwafanya wawe huru kukutafuta muda wowote ule wanapohitaji huduma ya usafiri.

7. Tumia programu ya teksi mtandao kama abiria

Unataka kujua madereva wengine wanafanya nini eneo katika eneo ulilopo? Unaweza kutumia programu ya abiria ya teksi mtandao.

Kuingia katika programu ya teksi mtandao kama abiria kutakuonyesha ni madereva wangapi wapo  katika eneo ulilopo. Hii itakusaidia kujua kama eneo ulilopo lina ushindani wa madereva wa teksi mtandao au la. Na kama eneo hilo lina ushindani, huna budi kwenda kujaribu katika maeneo mengine.

8. Fuatilia matukio maalum

Kuna wakati bei ya nauli huongezeka. Matukio maalum yanaweza kuwa kichocheo kikubwa cha mahitaji makubwa ya usafiri. Tamasha, kwa mfano, husababisha umati wa abiria waliokwama, waliochoka na  wanaotaka kuondoka na usafiri wa kwanza unaopatikana kwa safari yao ndefu ya kurudi nyumbani.

Kwa kweli, kuna mapungufu ya kuongezeka kwa hafla pia. Unaweza kutarajia kufungwa kwa barabara nyingi – bila kusahau muda unaotumia kusubiri kwenye trafiki.

Ikiwa ungependa pesa nyingi kwa muda mfupi, elekeza macho na masikio yako katika  matukio maalum. Kwa njia hiyo, unaweza kuamua kuwa katika eneo hilo mara tu shamra shamra zinapoanza. 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *