Magari yanayokubaliwa kusajiliwa uber

MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER TANZANIA 2022.

Uber ni kampuni inayoongoza katika sekta ya usafiri wa kushiriki yaani ride sharing /ride hailing. Maelfu ya watanzania madereva na wamiliki magari yanayokubaliwa kusajiliwa Uber wamekuwa wakitengeneza kipato kikubwa kwa kutoa huduma ya usafiri kwa abiria wa jukwaa hili.

Ingawa fursa hii ni nzuri sana na inafaa kila mtanzania mwenye uwezo aweze kunufaika nayo, inavyo vigezo na masharti muhimu ambayo ni lazima kufikiwa ili kukubaliwa kujisajili na kuanza shughuli.

VIGEZO VYA MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER

Kwanza kabisa ni lazima magari yafuate vigezo vya kuruhusiwa kuendeshwa nchini Tanzania. Kwa hiyo kabla ya kuanza kufikiria kuanza kazi Uber hakikisha gari lako lina nyaraka kamili maalumu na halali za serikali.

1. TOLEO LA GARI

Hii ni rekodi ya mwaka ambao gari limetenegenezwa. Magari ya matoleo mapya huwa na ubora zaidi kuliko magari yaliyotengenezwa zamani sana. Hii ni kwasababu kadri sayansi na teknolojia inavyokua ndivyo mainjinia wanavyozidi kujifunza na kuongeza ubora kwenye vyombo vya moto.

Kampuni ya uber ina kikomo cha magari toleo la mwaka 2003 au mapya zaidi na si chini ya hapo. Kama wewe ni dereva na unategemea kuendesha gari la mtu mwingine basi hakiki ni mwaka gani toleo la gari hilo lilianza kuuzwa kabla ya kujisajili kwenye tovuti ya Uber.

2. UKUBWA WA INJINI

MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER TANZANIA 2022.

Kampuni ya uber inaruhusu magari yenye ukubwa wa injini usiozidi 1300cc au Lita 1.3. Zipo njia tofauti za kuifahamu size ya injini ya gari yako kwa mfano:

  • Stika au maandishi juu ya injini ukifungua hood ya gari lako.
  • Kijitabu cha user manual ya gari huwa kina rekodi zote za gari
  • Kwa kutumia Vin number ambayo ipo kwenye manual ya gari (Kwa kawaida namba ya 5 hadi ya 9 ndiyo namba ya injini)
  • Kuuliza fundi wa magari garage akuelekeze

3. HALI NZURI

Magari yanayoendesha abiria wa Uber yanatakiwa kuwa na hali nzuri kikazi/kiufundi pamoja na kimuonekano. Hautakiwi kusajili gari bovu au lililoharibika na kuwa na muonekano mbaya kwasababu hii ni biashara.

Abiria wanapenda kusafirishwa kwenye gari zuri kwa ajili ya usalama na sio muonekano tu.

4. KADI SAHIHI YA GARI

Watu wengi huwa wanafikiri wanaweza kutumia gari zozote hasa gari binafsi kutengeneza pesa kupitia kubeba abiria wa Uber. Lakini kwasababu Uber ni biashara, kadi ya gari lako inabidi iwe ya gari la biashara na plate number inatakiwa iwe nyeupe na sio ya njano.

Kama gari lako ni private na unataka kuanza kuendesha abiria Uber basi unaweza kufata hatua zifuatazo kubadilisha kadi na plate number.

Jinsi ya kubadilisha kadi ya gari na plate number kutoka binafsi kuwa ya biashara.

  • Andika barua ya maombi ya kubadilisha kadi ya gari kutoka “Private” kuwa “Commercial”
  • Peleka barua kwenye ofisi za TRA ukiambatanisha kopi ya kitambulisho mfano cha NIDA, Passport size photo moja na uwe na kadi original ya gari hilo.
  • Utalipia Tsh 50,000/= kwa ajili ya uchapishaji wa kadi mpya.
  • Baada ya kupata kadi, ipeleke kwenye makampuni maalumu ya kuchapisha plate number ukiwa pamoja na kitambulisho chako mfano cha NIDA au kitambulisho cha mpiga kura.
  • Lipia gharama za kutengenezewa plate namba mpya.

5. BIMA YA BIASHARA

Magari yote yanayokubaliwa kusajiliwa Uber lazima yanakuwa na bima ya biashara na si binafsi. Baada ya kubadilisha kadi ya gari na plate namba kama ulivyoona hapo juu unatakiwa kulipia bima ya gari la biashara.

Bila hii hairuhusiwi kutumia gari lako kubeba abiria hata kama tayari una plate namba nyeupe.

6. STIKA YA HALMASHAURI YA JIJI

Kuwa na stika ya jiji ni kitu kingine cha muhimu kwa gari lako kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Uber. Stika hizi utolewa na halmashauri ya jiji na hulipiwa kwa mwaka.

MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER X

Hii ndio huduma inayopendwa zaidi kwasababu abiria wanaweza kuwa zaidi ya mmoja (kikundi/familia) wakielekea sehemu moja . Magari yanayokubaliwa kusajiliwa Uber X yanatakiwa kwanza kutimiza masharti 6 yaliyotajwa juu pamoja na yafuatayo.

7. IDADI YA MILANGO

Magari yanayoruhusiwa kuendesha Uber X yanatakiwa kuwa na milango minne kwasababu yanasafirisha hadi watu wanne kwa wakati mmoja. Magari mengi yanakigezo hiki lakini yale machache kama malori, hiace, Toyota Noah hayaruhusiwi ingawa yangeweza kubeba abiria wengi zaidi.

8. IDADI YA SITI

vigezo vya kujisajili kuendesha uber

Magari yote ya Uber X yanatakiwa kuwa na siti za kutosha watu wanne na ya Uber XL siti za watu 7 bila kuhesabu siti ya dereva.

9. STIKA NA NEMBO

Hairuhusiwi magari yoyote yenye stika zenye logo za makampuni mengine au makampuni ya serikali au hata stika ya Taxi kuendesha abiria wa Uber. Hakikisha unatumia gari ambalo halina nembo yoyote ili maombi yako ya kuendesha Uber yakubaliwe.

10. MAGARI YALIYOUNGWA UNGWA

Salvaged au rebuilt cars yaani magari ambayo yamebadilishwa vifaa vikubwa na kutengenezwa upya kwa kutumia vifaa vya gari tofauti hayaruhusiwi kuendesha abiria Uber.

Magari yanayoruhusiwa ni yale ambayo yapo na vifaa vyake kamili original vilivyoandikwa kwenye user manual mmiliki anayopewa wakati wa kununua. Hii yote ni kuhakikisha ubora na vyombo na usalama wa abiria.

LIST YA MAGARI YANAYOKUBALIWA

MAKEMODEL
ToyotaCame, Ractis, Fun Cargo, bB, ist, Platz, Yaris, Belta, Passo, Vitz, Duet
SuzukiSwift, Alto, Cervo, Kei, Wagon R, Every
NissanMarch, Micra, Note
VolkswagenPolo
MazdaAxela
DaihatsuTerios, Boon
VauxhallAstra
Mfano wa magari yanayoruhusiwa kusajiliwa Uber.

Kama gari lako lina viwango na linaheshimu vigezo vyote vya magari yanayokubaliwa kusajliwa Uber, ni vizuri ukafahamu jinsi ya kujisajli Uber ili uanze kutengeneza pesa nyingi kwa kutumia magari yako!.

Kwa maelekezo zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya UBER, chagua lugha unayoipenda na usome zaidi na usome zaidi kuhusu vigezo vya magari kuendesha abiria kwenye jukwaa hili.

Au SOMA HAPA namna ya kujisajili kama dereva au kusajili magari Bolt pia ili kuongeza kipato kikubwa zaidi!

7 thoughts on “MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER TANZANIA 2022.”

  1. Pingback: JINSI YA KUTENGENEZA PESA NYINGI KWENYE UBER/BOLT %

  2. Pingback: JINSI YA KUPUNGUZA GHARAMA YA MAFUTA YA GARI -

  3. Pingback: JISAJILI KUWA DEREVA UBER NA KUBALIWA HARAKA!

  4. Pingback: AINA ZA MAGARI YENYE FAIDA ZAIDI UBER TANZANIA 2022

  5. Kama kuna gari naombeni naona bora kupambana na kidogo ipo siku kitakua natafuta gari hesabu au mkataba no yangu 0748104080

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *