Kama wewe ni mdau wa sekta hii ya usafiri kwa njia ya programu utakuwa tayari unafahamu kuwa madereva wa Linkee Tanzania wanapata faida nzuri sana kupitia biashara hii ya usafirishaji.
Linkee ni kampuni mpya ya ride hailing ambayo imeingia kwenye biashara yenye wachezaji wakubwa sana kama Uber na Bolt.
Kutokana na hili, kampuni hii imeanza shughuli zake kwa kutoa motisha nyingi ili kuvutia madereva kujisajili na kusafirisha abiria wao.
Kampuni ya Linkee ilianza kusajili madereva kuanzia tarehe 25/11/2021 na app ilianza kuunganisha abiria kwa madereva kuanzia 29/11/2021 kupitia jukwaa la android.
Kuanzia mwezi Januari 2022 app ya linkee ilizinduliwa rasmi kwenye jukwaa la ios hivyo kusaidia watumiaji wa simu aina ya iPhones nao waweze kufurahia huduma za Linkee.
Kama ambavyo imeshatajwa hapo mwanzo, kampuni yoyote ikianzishwa huwa inafanya promotion kubwa ili kuvutia wateja. Kampuni ya Linkee pia imefuata kanuni hii kwa kuanza shughuli zake huku ikitoa motisha kubwa sana kwa madereva kama ambavyo utaenda kuona.
MOTISHA 9 AMBAZO MADEREVA WA LINKEE TANZANIA WANAPATA.
1. HUDUMA BURE
Kama tunavyofahamu makampuni ya usafiri huu aina ya ride hailing hutengeneza pesa kwa kuchukua sehemu ya kipato cha dereva kama malipo ya kumpatia dereva abiria.
Madereva wote wa makampuni mengine hukatwa kiasi hiki katika mapato yao pia kama ada ya kulipia ile huduma ya kutumia teknolojia hii ya kuunganishwa na abiria.
Kampuni ya Linkee ilitangaza kuwa miezi 6 tangu huduma zao zianzishwe madereva hawatakatwa hela yoyote kwa ajili ya kulipia jukwaa.
Hii inamaanisha kuwa kuanzia mwezi wa Novemba 2021 hadi mwezi May 2022 madereva wa Linkee Tanzania watakuwa wakifurahia kupata nauli yote bila makato!.
2. KAMPUNI IPO TANZANIA
Jukwaa la usafiri la Linkee limetengenezwa Tanzania kwa ajili ya Tanzania. Hii ina maanisha kuwa wamiliki wanafahamu changamoto za usafiri kwa abiria pamoja na changamoto za madereva wa ride hailing Tanzania.
Linkee imeweza kutumia muda mrefu kuchanganua changamoto za madereva wa kwenye majukwaa mengine ya usafiri. Uongozi wa kampuni hii umetamka mara nyingi mbele waandishi wa habari kuwa moja ya lengo lao kubwa ni kuhakikisha madereva wao wanatengeneza kipato kizuri kinachoendana na bidii zao.
Kwasababu kampuni ni mpya na imeundwa mahususi kwa ajili ya Tanzania, kunatokea urahisi zaidi wa kuwasiliana na uongozi, kutatulika matatizo kwa haraka na kupunguza matatizo mengine ambayo hutokea mara nyingi katika makampuni ambayo yapo mbali sana na watumiaji.
3. URAHISI WA KUJISAJILI
Kampuni ya Linkee imefanya hatua ya kuomba kuwa dereva kuwa rahisi ili kuhakikisha kila mtu anayekidhi vigezo anapata fursa bila ugumu.
Unachotakiwa ni kudownload app na ku SWITCH kwenda “DRIVER MODE”. Baada ya hapo unaweza kupakia nyaraka zote zinazotakiwa moja kwa moja kupitia app. Katika makampuni mengine kama Uber na Bolt ni lazima kujisajili kupitia tovuti zao mtandaoni.
Nyaraka dereva anazotakiwa kupakia ni leseni, picha ya profile, kadi ya gari, bima ya gari pamoja na picha ya gari.
4. KUKUBALIWA HARAKA
Kwasababu kampuni bado ni mpya na waombaji bado sio wengi sana, hatua ya nyaraka kukaguliwa na kukubaliwa huchukua si zaidi ya masaa 24. Hii husaidia dereva kuweza kuanza kazi chap chap na kuanza kutengeneza pesa.
5. KUCHAGUA NAULI
Madereva wa Linkee wanaweza kuchagua nauli tofauti kutegemeana na umbali wa safari, aina ya eneo anapoelekea abiria na muda wa siku.
Hii ni tofauti na kampuni nyingine kama Uber ambapo dereva hata hafahamu abiria anaelekea wapi mpaka akubali safari na amfikie abiria.
Pia kwenye jukwaa la Linkee hakuna adhabu ya kupunguziwa alama pale ambapo dereva anakataa safari sana kama kweye jukwaa la Uber.
6. UKARIBU WA MADEREVA
Kampuni ya Linkee ina group la whatsapp maalumu kwaajili ya madereva wote pamoja na lingine kwa ajili ya abiria. Lengo kuu ni kuwaunganisha madereva waweze kushauriana na kufahamiana.
Pia lengo lingine la muhimu kabisa ni kuleta urahisi wa mawasiliano kati ya madereva na uongozi. Pale ambapo dereva anakuwa na malalamiko yoyote kuhusu kampuni ni rahisi kuyafikisha kwa wahusika na kusababisha utatuzi wa haraka zaidi.
Sio lazima kwa kila dereva ajiunge kwenye group hili. Lakini ni kitu muhimu sana ambacho inafaa kujaribu na kunufaika nacho. Kama dereva akipenda kujiunga anaweza kuingia kwenye group kwa kutuma ujumbe kwa namba ifuatayo na kuomba wamuunge:
7. ZAWADI POINTS
Madereva wa Linkee Tanzania hupewa za wadi kwa mfumo wa points ambazo wanaweza kuzitoa kama pesa kupitia simu au kununulia data za internet.
Kwa mfano kila dereva mpya anapomaliza usajili na kukubaliwa kuendesha basi hupata pointi 3,500. Dereva mpya anapokamilisha safari yake ya kwanza hupata pointi 11,500. Pia zipo njia nyingine mbalimbali za kupata pointi kama kuwa na alama nzuri kutoka kwa abiria nk.
Pointi 3,000 za Linkee ni sawa na tsh 3,000/= ambazo unaweza kutoa kama pesa au ukanunulia bundle la internet!.
Ili kupata pesa zako za pointi au kununua data unachotakiwa kufanya ni kuingiza taarifa zako za simu kwenye app na uchague ni kiasi gani cha pointi zako unataka ziingizwe kwenye salio lako kama pesa au kama bundle.
8. TENGENEZA PESA KWA KUALIKA MADEREVA WENGINE
Kampuni ya Linkee ina mpango mzuri sana wa kuongeza kipato kwa kupata zawadi za pointi kupitia kualika madereva wengine au hata abiria wajisajili kutumia app ya Linkee.
Kwasababu kampuni bado ni mpya hii ni fursa kubwa sana kwasababu kuna watu wengi sana ambao watakubali kutumia link yako kujisajili na hivyo wewe kupata kipato nje ya kuendesha gari.
Dereva anaweza kupata point 6,000 sawa na tsh 6,000 kwa mtu atakayejiunga kwa kupitia link a code yake kama abiria. Pia hupata point nyingi zaidi kila dereva mpya anapojisajili kwa link yake.
Kwa kila dereva anayejiunga kupitia wewe unapata:
- Pointi 100 mtu akijisajili kwenye app
- Pointi 6,500 maombi yake yakikubaliwa
- Pointi 5,000 akikamilisha safari ya kwanza
Jumla pointi 11,600 kwa kila mmoja ambayo ni karibia na tsh 12,000/=.
SOMA ZAIDI KUHUSU ZAWADI POINTS KUPITIA TOVUTI YA LINKEE HAPA NA HAPA.
9. USALAMA
Kampuni ya Linkee imechukua hatua kubwa katika kuhakikisha usalama wa madereva na abiria. Katika application ipo njia ya kuweza ku connect watu wako wa karibu waweze kutrack location yako wakati wa safari ili kujua mahali ulipo muda wote.
Pia kuna kitufe cha msaada au “SOS” ambacho kimeunganishwa moja kwa moja kwa polisi. Hivyo unapopata hatari ya ghafla na ukakibonyeza basi taarifa zinaenda polisi na wataweza kukufata pale pale ulipo kukupa msaada.
Bila shaka madereva wa Linkee Tanzania wanafaidi manufaa mengi kutokana na upya wa kampuni. Kama ambavyo tumejadili katika makala nyingine hapa Weibak, ni vizuri kwa madereva kuweza kujisajili katika majukwaa mbalimbali ili kuongeza uwezekano wa kupata abiria pale ambapo wapo chini kwenye jukwaa fulani.
SOMA: FANYA HIVI KAMA HAUPATI ABIRIA UBER/BOLT.
Faida nyingi zipo Linkee na hatua za kujisajili ni fupi na za haraka, hivyo hakuna ubaya kama madereva wengine wangeweza kujiunga na kujionea kama kweli faida za huku zinawafaa.
Je, umeshajisajili kuendesha abiria Linkee? Kama ndio tafadhali tuambie, huko umefurahia manufaa gani?
Nahitaji akaunti ya bolt
Habari Ndugu Meshack Malite, pitia chapicho letu hili litakusaidia kufahamu jinsi ya kupata akaunti ya bolt.
https://weibakcarsharing.com/jisajili-kuwa-dereva-bolt/
Office zenu ziko wapi
Kwa sasa unaweza wasiliana na sisi kupitia mitandao ya kijamii au kupitia barua pepe [email protected] / [email protected]
karibu sana