Kila dereva Uber/Bolt anapoanza kazi ya kuendesha abiria kwenye majukwaa hayo huambiwa kuwa anahitaji gari, ujuzi na smartphone tu kujisajili.
Ingawa hivyo vinaweza kutosha, utakuja kugundua kwamba abiria hawatabiriki. Kwa hiyo ni vizuri sana kuwa tayari kwa jambo lolote linaloweza kutokea wakati wa safari.
Katika makala hii utaenda kujionea vifaa muhimu sana ambavyo kila dereva anapaswa kuwa navyo ili kuhakikisha mambo yanaenda murua. Kumbuka, si lazima kuwa navyo vyote lakini ukiwa navyo vingi zaidi vitakunufaisha zaidi.
KILA DEREVA UBER/BOLT ANAPASWA KUWA NA VIFAA HIVI
1.HOLDER YA SIMU
Hiki ndio kifaa muhimu kuliko vyote kwasababu kinatakiwa kutumiwa wakati wote ili kuhakikisha usalama wa dereva na abiria. Zipo aina mbalimbali ambazo unaweza kuchagua kulingana na upendeleo na uwezo wako.
Bonyeza hapa kuangalia baadhi ya phone mounts na bei zake.
FAIDA:
- Kinasaidia dereva kuona direction kwenye simu bila kuinama inama hivyo kuhakikisha usalama barabarani.
- Abiria hutoa alama nyingi kwa madereva wenye phone mount kwasabau nao wanaweza kuona uelekeo kupitia simu ya dereva. Pia hujisikia amani kuendeshwa na dereva ambaye macho yake yapo barabarani muda wote na si mkononi kwenye simu.
- Kuepusha kukamatwa na traffic police: Madereva wanahitaji kufata direction kwenye simu lakini sheria hairuhusu kuendesha huku ukitumia simu. Ukiwa na phone holder unaweza kuendelea kuangalia maelekezo ya kwenye app bila kuishika simu hivyo unakuwa hauvunji sheria.
2.CHAJA YA SIMU
Haiwezi ikapita siku bila abiria kuulizia kama una charger ya simu. Kwa barabara zetu hasa kwenye miji mikubwa kama Dar es salaam, safari fupi inaweza kuwa ndefu kwasababu ya foleni.
Hivyo mara nyingi abiria hupenda kuchaji simu zao kwenye gari ili kuhakikisha watakuwa na charge ya kutosha ya kuagiza usafiri tena wakati wa kurudi.
Ni muhimu sana kwa kila dereva Uber/Bolt awe na kifaa cha kucharge simu zaidi ya moja kwa wakati mmoja, ili kila abiria kwenye gari aweze kucharge simu bila kusubiriana.
Pia ni muhimu kuwa na USB cable za aina tofauti ili kuhakikisha aina nyingi za simu zinaweza kupata huduma.
Kama kawaida hiki kifaa nacho kina faida kwa wote abiria na dereva. Kwahiyo itakuwa vizuri kama utakuwa nacho na itakupatia ratings nzuri pia kutoka kwa abiria wako.
3. KAPETI LA GARI
Ukipakia abiria wanaotoka ufukweni au wanaoishi maeneo yenye matope hasa wakati wa mvua nyingi kapeti la gari lako litakuwa linachafuka sana. Hii itakuwa inakupa mtihani wa kusafisha mara kwa mara badala ya kujikita kwenye kuendesha zaidi.
Kila dereva anatakiwa kuwekeza katika makapeti ya rubber kwasababu ni marahisi sana kusafisha uchafu wowote kwa haraka. Kapeti za rubber ni kama aina ya plastiki kwa hiyo hakuna haja ya kupoteza kuda kuzifua na kusubiri masaa mengi zikauke.
Unaweza kuzimwagia maji tu na kuzifuta kisha kuzitandika tena hivyo kuhakikisha usafi muda wote.
4.CAMERA
Camera za kwenye gari ni muhimu kama insuarance ilivyo muhimu. Kila dereva Uber/Bolt anapaswa kuwekeza kwenye Camera nzuri ya kwenye dashboard.
FAIDA:
- Ushahidi: Unapopata matatizo kama ajali barabarani camera yako itakusaidia kuonesha kuwa hauna hatia hivyo kukuepushia hasara. Pia ukipata abiria ambaye atakuletea matatizo kama kukuvamia, kukuibia, kuleta fujo au uharibifu utaweza kupeleka video yako kwa uongoozi wa Uber/Bolt au Polisi ili kupata haki yako.
- Utulivu: abiria wako wakiingia kwenye gari na kuona kuwa kuna camera wataogopa kukuletea matatizo kwa hiyo watakuwa watulivu safari nzima.
- Furaha kwa abiria: Camera ya kwenye gari lako itafanya abiria wako wawe na amani kwasababu watakuwa wanajua kuwa wewe hauwezi kuwafanyia ubaya huku camera ipo. Pia watakuona professional na wataweza kukupa ratings kubwa hivyo kukusaidia kuwa maarufu na kupata wateja wengi zaidi.
Zipo aina nyingi sana za camera za kwenye magari ambazo unaweza kuzipata kwa bei nzuri tu. Unaweza kudhani ni kiasi kikubwa cha kuanza nacho lakini faida yake ni kubwa sana kuzidi hata huo mtaji wa kununulia hiyo camera.
5.TOWEL NA TISSUE PAPERS
Mataulo ni muhimu sana katika magari yote yanayosafirisha abiria hasa kipindi cha mvua. Kazi yao muhimu ni kufuta vimininika na pia kutandika kwenye siti kabla abiria aliyelowa na mvua kukaa ili kuzuia viti kulowa.
6.KAVA ZA SITI
Kwanza kabisa kava zinaleta muonekano mzuri sana wa gari! Pili zinalinda siti zisiharibike au kuchafuka kwa kukaliwa mara kwa mara na kumwagiwa vitu kama soda, michanga nk
7.VIFAA VYA USAFI
Gari lako ni kama ofisi yako, kwa hiyo wateja wako wanatakiwa kulikuta likiwa safi na lenye harufu nzuri. Kutokana na hili kila dereva Uber/Bolt anashauriwa kuwa na vifaa vichache vya usafi kama brush/duster/ fagio ndogo za gari na air freshener.
Pia unaweza kuwa na ki-dustbin kidogo cha kwenye gari ili kuepusha abiria kutupa uchafu ndani au nje ya gari. Unaweza pia kuwekeza kwenye vi-vacuum machine vidogo vya kwenye grari. Hivi husaidia kuondoa vumbi hasa kama huwa unapata safari za barabara za vumbi.
8.MIFUKO
Kama hauna dustbin unaweza kuweka mifuko kwa ajili ya kukusanyia uchafu kwenye gari. Lakini pia mifuko ya plastic ni muhimu sana hasa wakati wa usiku kwasababu ikitokea abiria amepataka kichefuchefu aweze kutumia mfuko badala ya kuchafua gari lako.
9.HUDUMA YA KWANZA
Huu ni mkusanyiko wa vifaa mbali mbali vinavyoweza kusaidia mtu akipata tatizo la kiafya ghafla. Unapokuwa unaendesha abiria usiowafamu ni muhimu sana kuwa tayari kwa lolote.
Muda wowote katika safari abiria anaweza kuumwa kichwa, tumbo, kupatwa kizunguzungu kwa kuishiwa sukari mwilini nk. Kwa hiyo ni muhimu sana kuwa na vifaa vichache tu vinavyoweza kuwasaidia kama vinavyooneshwa hapa chini:
- Dawa za maumivu mfano Paracetamol, dawa tatu, hedex nk
- Glucose kwa mtu aliyepungukiwa sukari
- Spirit ya kusafisha mchubuko wa ngozi
- Pamba ya kusafishia na kupakia spirit
- Plasta za kufunika mchubuko wa ngozi au kidonda
- Antihistamines kwa ajili ya kutibu allergy haraka
- Maji ya kunywa
Kuwa na vitu hivi ni muhimu kwasababu vitasaidia sio abiria wako tu bali na wewe mwenyewe pale unapopatwa na tatizo.
10.NGUO YA ZIADA
Ili kuhakikisha unakuwa smart na professional muda wowote ni vizuri wewe kama dereva uwe angalau na nguo ya juu ya ziada. Pale ambapo utachafuka bahati mbaya unaweza kubadilisha tu na kuendelea kuonekana mtanashati bila kupoteza muda kwenda nyumbani kubadilisha.
11.MASKS NA SANITIZERS
Tangu janga la ugonjwa wa uviko 19 lianze imekuwa ni lazima madereva pamoja na abiria kuwa makini sana katika kujikinga.
Hakuna kitu kibaya kama kuumwa kwasababu ujuzi wako wa kazi ndio mtaji wako. Kwa hiyo ili kuhakikisha unatumia fursa hii kikamilifu jitahidi sana kujikinga na Uviko kwa kuvaa mask, kutumia sanitizer na kuwa na vya ziada muda wote hasa ukipata abiria ambaye hana mask.
Kwa ufupi vifaa hivi ni muhimu sana kwasababu vinafaidisha abiria ambao ni wateja wako lakini vinakusaidia na wewe pia. Si lazima utumie pesa nyingi sana kupata kila kimoja, unaweza kuvipata kwa bei nzuri tu ukitumia muda wa kutosha kulinganisha bei kwa wauzaji tofauti
Kama vile bado haujaanza kuendesha abiria Uber/Bolt usingoje zaidi! SOMA HAPA jinsi ya kujisajili kuwa dereva wa Uber.
AU ANGALIA HAPA jinsi ya kujisajili kuanza kutengeneza pesa kwa kuendesha chombo chako Bolt. Kisha anza kwa kujifunza HAPA jinsi ya kutengeneza 500,000/= tsh na zaidi kwa kuendesha abiria kwenye majukwaa haya na mengineyo.
Pingback: JINSI YA KUTENGENEZA PESA NYINGI KWENYE UBER/BOLT %