Kanuni za LATRA

KANUNI ZA LATRA KWA MAKAMPUNI NA MADEREVA MTANDAONI

Kanuni za LATRA zilizoanza rasmi 16 April 2022 zimeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya programu za safari Tanzania. Watu wengi wamesikia sheria moja tu ya kimo cha kamisheni au ada ya 15% kwa madereva lakini hiyo siyo sheria pekee iliyowekwa.

Mamlaka ya udhibiti wa usafri wa nchi kavu LATRA ilianzishwa chini ya kifungu namba 4 cha sheria ya udhibiti usafiri wa nchi kavu mwaka 2019.

Mwaka 2019 Latra ikiwa na mamlaka ya kuthibiti usafiri pamoja na kukagua na kudhibiti kiasi cha nauli, ilipitia nauli za huduma za programu za usafiri ambazo zilianza rasmi mwaka 2020 Tanzania bara.

Tayari utakuwa unafahamu kuwa kampuni za usafiri kwa programu za usafiri zilianza Tanzania hata kabla Latra haijaundwa.

Kwa mfano Uber ilianza 2016, Bolt ilianza mwaka 2017, Ping mwaka 2019 pamoja na kampuni ya kikenya ya Little ride ambayo ilianza March 2019.

Kipindi hicho cha kabla ya LATRA, utaratibu uliokuwepo ni kwamba mamlaka za serikali za mitaa ndio zilikuwa zikisimamia huduma za taxi na programu za usafiri. Lakini chini ya utaratibu huo, hapakuwa na taratibu za wazi za kudhibiti huduma za teksi au za programu za safari.

Kwa hiyo kuanzia Aprili 2020 LATRA ilianza udhibiti wa usafiri ambapo ulipitia na kuamua kimo cha nauli pamoja na kusimamia watoa huduma wafate sheria.

Misingi ya kanuni za LATRA kwenye nauli za usafiri.

Mabadiliko ya nauli na makato au kamisheni yanayofanywa na LATRA huwa yanazingatia misingi maalumu ili kuhakikisha kuwa watumia huduma na wamiliki wanapata faida wanayostahilli bila mmoja kuonewa.

1. Gharama za uendeshaji

Kampuni za programu za safari ni kubwa na zinahitaji utaalamu na uendeshwaji wa hali ya juu sana. Ukiacha madereva ambao wamepata fursa ya kujiajiri, makampuni haya yana wafanyakazi wake wengi sana wanaofanya kazi kubwa nyuma ya pazia kuhakikisha kuwa majukwaa ya usafiri yanakuwa na ubora wa kufaa kutoa huduma.

Hii ni tofauti kubwa sana ukilinganisha na sekta nzima ya usafiri wa teksi za kawaida. Kwa hiyo mamlaka inapopitia na kuamua viwango vya bei huwa inahakikisha kuzingatia gharama za kuendesha kampuni hizi.

SOMA: Tofauti kati ya Taxi za kawaida na Programu za safari (Taxi za mtandaoni)

2. Mitambo ya kiteknolojia

Kampuni za programu za safari hutumia teknolojia katika kurekodi mienendo ya madereva pamoja na mitambo ya kukokotoa nauli. Hii yote huhitaji kiasi kikubwa cha fedha ili kuweza kufanya kazi kwa usahihi muda wote.

3. Umbali na muda

Kampuni za ride hailing hutumia vigezo vya umbali na wakati kukokotoa nauli za huduma zao. Kutokana na hili Mamlaka husika nayo inafata vigezo hivi ili kuhakikisha wadau wanapangiwa nauli ambayo ni sahihi na yenye usawa.

4. Vigezo vya kiuchumi

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu huzingatia sana mabadiliko ya kiuchumi wakati wa kupitia na kuamua nauli na viwango vya kamisheni.

Hii ni kwasababu nchi yetu hupitiia vipindi vya uchumi kuyumba kwa kiasi kikubwa hivyo kuweza kupelekea uwezekano wa kupoteza usawa hasa kwa makampuni yanayotokea nchi za uchumi tofauti.

Vigezo vya uchumi kama vile viwango vya ubadilishaji fedha (exchange rates), kushuka kwa thamani pamoja na mfumuko wa bei huzungatiwa na LATRA kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya mwisho.

5. Kodi na ada za kisheria

Kiasi cha nauli na kamisheni hukokotolewa pia kwa kuzingatia kodi inayolipwa na mtoa huduma pamoja na ada wanazolipia kwa ajili ya kupata vibali mbali mbali.

Inaweza kuwa haulifahamu hili lakini makampuni yote ya programu za safari hulipa ada mbali mbali kwa uongozi wa jiji wanalotolea huduma kama ada ya uendeshaji. Nchi nyingi sana zenye makampuni haya zimetoa ripoti kuhusu jinsi ada hizi zimeweza kusaidia kuendeleza majiji yao.

Kwa hiyo hizi gharama zote huzingatiwa ili kuhakikisha kampuni hazipati hasara na kuamua kuacha kutoa huduma.

6. Miundombinu na msongamano barabarani

Nauli za huduma za programu za safari huwa rahisi kwenye nchi zenye miundombinu na barabara nzuri. Hii ni kwasababu kampuni hizi hutumia vigezo vya umbali na muda katika kukokotoa kiasi cha gharama.

Katika nchi yetu kuna changamoto kubwa sana ya barabara zisizo na ubora pamoja na foleni za kupitiliza. Kwasababu hii hufanya makampuni kutumia fedha zaidi kuendesha huduma hizi ambazo huwa zinazochelewa. Yaani kwa umbali ule ule dereva Uber aliye Marekani hufika haraka zaidi hivyo kutumia teknolojia kwa muda mfupi kuliko dereva wa Dar ambaye hukwama kwenye foleni.

Kwa hiyo mamlaka huzingatia hili pia katika kuamua nauli na makato ili kutosababisha makampuni kuendesha biashara kwa hasara tu.

Gharama nyingine ni mahitaji ya usalama. Makampuni haya ya usafiri hutakiwa kuwa na huduma fulani za usalama kwa mfano huduma za kupiga simu polisi, bima ya ajali, ulinzi au huduma ya SOS yaani kuomba na kupata msaada wa haraka. popote.

Hizi zote hugharamiwa na kampuni husika hivyo hutakiwa kufikiriwa wakati wa nauli na kamisheni zinapoamuliwa.

7. Uwezo wa kumudu huduma

Latra huhitaji kuhakikisha kuwa kiasi cha nauli kinaendana na hali ya uchumi ya wananchi wengi. Pia kiasi cha makato ya madereva kisiwe kikubwa sana kupitiliza hali ya kiuchumi ya madereva wengi Tanzania.

MAAMUZI YA BODI

Katika kikao cha 6 cha bodi kilichofanyika 27 Januari 2022, bodi ilipitisha kanuni za LATRA zifuatazo katika nauli za programu za safari.

Nauli ya kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa tano usiku ( 05:00:01 – 23:00:00 )

KipengeleKiasi Tsh
Nauli kwa umbali wa kila mita 10079.16
Nauli kwa muda wa kila sekunde 3641.47

Nauli ya kuanzia saa tano usiku hadi saa kumi na moja asubuhi (23:00:01 – 05:00:00)

KipengeleKiasi Tsh
Nauli kwa umbali wa kila mita 10083.12
Nauli kwa muda wa kila sekunde 3643.54

Kwa kuzingatia haya nauli zilizo pitishwa ni kama ifuatavyo

(a) Nauli ya pogramu za safari ni TZS 900.00 kwa kilomita.

(b) Nauli ya programu za safari ni TZS 100.00 kwa dakika.

Kiwango cha chini cha nauli kilichopitishwa

Kiwango cha chini cha nauli ni TZS 3,000.00. hii inamaanisha kusiwe na safari za chini ya tzs 3000/=

Kiwango cha juu cha ada ya huduma kilichopitishwa

Kiwango kilichokubaliwa ni 15%.

Hii inamaanisha madereva hawaruhusiwi kukatwa zaidi ya asilimia hizo kutoka kwenye nauli.

KANUNI ZA LATRA ZA ZILIZOONGEZWA KWA AJILI YA MADEREVA NA MAKAPUNI YA PROGRAMU ZA SAFARI.

1. Kanuni ya majukwaa

Makampuni yanatakiwa kutumia majukwaa ya usafiri ambayo yana uwezo wa kupeleka taarifa maalumu moja kwa moja kwa mamlaka.

Hii inamaanisha kuwa kuwepo na application integration interphase ambayo kwa lugha rahisi ni muunganiko wa kiteknolojia kati ya app za safari na miundombinu ya LATRA.

Hii itasaidia mamlaka kuweza kusimamia na kuchunguza kampuni muda wowote bila hata kuomba taarifa kutoka kwao.

2. Kuondoa changamoto ya kufata abiria wa mbali

Wenye majukwaa wanatakiwa kuhakikisha wanatumia mitambo yao vizuri kuchagua magari yaliyo karibu zaidi na abiria kutoa huduma badala ya dereva wa mbali kufata abiria na kutolipwa fidia.

Madereva wengi sana wamekuwa wakilalamikia sana tatizo hili kwa hiyo kuanzia 16 Arpili 2022 halitakiwi litokee.

3. Ustraarabu

Kwa muda mrefu abiria wamekuwa wakilalamika sana kuhusu kauli mbaya za baadhi ya madereva. Hii imefikia hadi kutokea kwa matukio ya kupigwa na kulazimishwa kulipa nauli ambazo ni zaidi ya zile inayoonekana kwenye jukwaa.

Kutokana na hili Latra imesisitiza watoa huduma kuepuka kutumia lugha ya matusi, kubadilisha bei na kuendesha magari machafu.

4. Madereva kusikilizwa

Wamiliki makampuni ya programu za safari wanatakiwa kuwapa madereza jukwaa la kusikilizwa hasa kama abiria wanalalamika sana juu ya huduma.

Makampuni mengi husikiliza na kuwapa kipaumbele abiria kuliko madereva. Hii inakuwa si vizuri kwasababu mara nyingi madereva nao huwa na changamoto zinazopelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi.

5. Ukaguzi wa mikataba

Mamlaka imeamuru wenye makampuni wote kuhakikisha mikataba yao na madereva ipelekwe kwa mamlaka kwa ajili ya kukaguliwa kabla haijaanza kutekelezwa.

Pia mikataba yote ni lazima ijumuishe maelekezo ya kina kuhusu promotion zote ambazo mdau anaweza kuzipata kwa kutumia huduma au kufanya kazi.

6. Watoa huduma hawaruhusiwi kutumia mbinu za kijanja kufanya mabadiliko yoyote ya mfumo wa shughuli za utoaji huduma, kukokotoa nauli na kupilia huduma.

7. Watoa huduma (madereva ) wanatakiwa kuzingatia misingi ya usalama na ulinzi.

Je unaonaje kuhusu kanuni hizi mpya za LATRA?

Je unadhani kumekuwa na unafuu wowote kwa madereva kutokana na mabadiliko haya?

Tushirikishe kwenye sehemu ya comment ili tuweze kubadilishana mawazo!.

4 thoughts on “KANUNI ZA LATRA KWA MAKAMPUNI NA MADEREVA MTANDAONI”

  1. Kunamadereva wamejisajili kwenyejukwa × gari wanazotumia siyo za biashara ni privet kwakukwepa kulipia vibari vya kufanyia biashara naombakujua mnatusaidia vipi ? Na mnawajuaje coz naona magarimengiyu privet hilazinafanya biashara ya mtandao angali awajakidhi vigezo ?

  2. Nimeshtuka sana kuona LATRA inatambua kila changamoto mpka ambazo sikudhani kama wanazifahamu hongereni kwa hilo
    Asa nashangaa kuona makampuni yana kokotoa nauli mpka 700 kwa km na ushahidi wa screenshot nnazo hapa ndio maana nikaamua nipitie tena kanuni hizi .

    Baadhi ya makampuni pia wanatoa bei kabla ya trip kuanza kama indriver na linkee tena ni discounted prices alafu unakuta unakaa kwenye foleni mda mrefu gari ipo silence na AC ipo on mafuta yanaenda halafu unapewa hela ile ile ya mwanzo bila calculation za muda wa safari kasababu bei ilioonekana mwanzo ni bei ya kilometa muda haujawa calculated

    Na hilo suala la mteja kuchagua dereva kama kwenye indrive mteja anachagua dereva wa mbali anaacha wa karibu hilo ni suala ambalo nimeona mmeliadhinisha wakati halifanyiwi kazi na baadhi ya makampuni

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *