Jisajili kuendesha uber kubaliwa haraka

JISAJILI KUWA DEREVA UBER NA KUBALIWA HARAKA!

Majukwaa ya usafiri wa kushirikiana yamefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri. Maelfu ya wamiliki magari na madereva waliochukua hatua ya kujisajilii kuwa dereva Uber wamekuwa wakitengeneza faida kubwa sana hadi kuhamasisha watanzania wengine wajiunge na fursa hii.

Katika makala hii utaenda kuona jinsi ya ku jisajili kuwa dereva Uber ili na wewe uanze kutengeneza kipato kupitia jukwaa hili lenye mamilioni ya madereva dunia nzima.

JISAJILI KUWA DEREVA UBER KWA KUFATA HATUA HIZI.

Kwanza kabisa kabla ya kuanza harakati za kujisajili ni muhimu kujiuliza maswali yafatayo:

  • Je una umri sahihi wa kuendesha gari?
  • Una leseni ya kuendesha gari?
  • Huduma za Uber zinapatikana kwenye mji uliopo?
  • Unamiliki gari?

Kampuni ya Uber ina vigezo kuu vinne ambavyo ni lazima vitimizwe ili kukubali mtu aanze kuendesha abiria.

1. KIGEZO CHA UMRI

Ingawa miaka 18 ndio umri ambao mataifa mengi yanaruhusu mtu kuanza kazi au kuendesha gari, Uber inahitaji dereva asiwe chini ya miaka 21.

Hii ni kwasababu kazi hii ya kuendesha abiria sio ya mchezo kwa hiyo ni muhimu madereva kuwa watu wazima na wenye busara.

2. UMILIKI WA LESENI.

Kila mwombaji wa kazi ya kuendesha uber lazima awe na leseni original kutoka kwa mamlaka husika .Pia kama dereva unatakiwa kuwa na experience /ujuzi wa kuendesha gari kwa mwaka mmoja na zaidi au miaka mitatu na zaidi kama umri wako ni chini ya miaka 23.

Hii inamaana Uber hufanya uchunguzi wa mwaka wako wa kupata leseni ili wajue umekuwa ukiendesha kwa muda wa miaka mingapi.

3. KIGEZO CHA ENEO/ LOCATION

Kabla ya kupoteza muda mwingi kuanza jisajili kuwa dereva wa Uber, hakikisha huduma hii ipo mahala unapoishi. Kwa Tanzania hadi sasa huduma hii inapatikana katika mji mmoja tu ambayo ni Dar es salaam tu.

Bonyeza hapa ili kufahamu nchi zote na miji yote Afrika na dunia nzima ambapo kampuni Uber inafanya kazi. Pia jisajili katika website yetu ili upate update zote kuhusu Uber na kama itaanza shughuli katika mji uliopo!

Lakini kama unaishi mji ambao bado Uber haijafika ipo njia nyingine ya kujiunga. Jisajili kuwa dereva Uber katika mji ambao kampuni ipo na ambao unaufahamu vizuri.

Hii ina maana unaweza kuhamia kwenye mji wowote unaoufahamu zaidi kati ya hiyo minne na kuanza kuendesha.

4. VIGEZO VYA MAGARI

Ili kuanza kazi ya kuendesha abiria uber wala hauhitaji kuwa na gari lako mwenyewe. Wapo madereva wengi wanaofanya shughuli hii kwa kuendesha magari ya wamiliki na kugawana nao faida nzuri sana.

Kama wewe ni mmiliki wa gari, bonyeza hapa ili uone vigezo ambavyo ni lazima gari lako lifikie ili uweze kukubaliwa libebe abiria wa Uber.

Kama hauna gari lakini wewe ni dereva mzuri unaweza kupata magari ya watu wengine na ukaanza kuendesha na kugawana faida na wenye magari.

Baada ya kujitathmini na kutambua kuwa vigezo vyote unavyo, sasa tuelekee moja kwa moja kwenye mchakato mzima wa kujisajili kwenye jukwaa la Uber.

A. ANDAA NYARAKA ZINAZOHITAJIKA

Ili kuweza kukubaliwa kuendesha abiria Uber unahitaji kuwa na nyaraka zifuatazo.

  1. Leseni ya udereva Class C1, C2 au C3.
  2. Picha ya dereva
  3. Bima ya gari commercial (ya biashara)
  4. Kadi ya gari la abiria.
  5. LATRA road licence
  6. Cheti cha tabia njema cha Polisi.

Ili kuokoa muda na kupunguza usumbufu ni vizuri kukusanya nyaraka zote muhimu kabla ya kuanza mchakato wa usajili.

LESENI CLASS C

Tanzania ina makundi 8 ya leseni za udereva ambayo yamepewa majina ya herufi A,B,C,D,E,F,G na H. Kundi A ni leseni za kuendesha pikipiki za aina tofauti (A1, A2, na A3).

Kundi B ni leseni za vyombo binafsi vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa, magari ya biashara na magari ya kutoa huduma kwa umma.

Kundi C ni leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma ambazo zipo aina 3 C1, C2 na C3. Aina hii ndiyo inahitajika ili uweze kuendesha abiria wa Uber na majukwaa mengine ya usafiri wa jumuiya.

Kundi D ni la leseni za kuendesha magari madogo ya mizigo ya biashara.

Kundi E ni kwa ajili ya kuendeshea magari makubwa ya mizigo ya biashara. Kundi/Class F ni leseni za za magari yanayokokota TRELA. Kundi G ni kwa ajili ya kuendesha magari ya shambani na migodini, na mwisho kundi H ni leseni ya muda kwa ajili ya wanaojifunza kuendesha magari.

Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu uchambuzi wa makundi ya leseni.

Si vibaya kama hauna Leseni kundi C kwasababu unaweza kubadilisha leseni yako kuwa C kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). Kisha jisajili kuendesha Uber na wewe uweze kutengeneza kipato kikubwa kutokana na ujuzi wako.

Fahamu hatua zote za kubadili leseni yako kuwa Class C pamoja na gharama zake.

PICHA YA DEREVA

Hakikisha upo katikati ya picha, kuna mwanga wa kutosha na hakuna vitu nyuma yako. Picha ioneshe vizuri uso mzima hadi mabega, usivae miwani ya jua wala usitumie picha ya kwenye leseni.

BIMA YA GARI

Bima ya magari la binafsi na magari ya biashara ni tofauti. Hakikisha gari lako au la mwajiri wako limekatiwa bima ya biashara ambayo haijaisha muda wake.

KADI YA GARI LA ABIRIA

Ili gari likubaliwe kuendesha abiria wa Uber ni lazima liwe na kadi ambayo inaonesha matumizi yake ni ya biashara na lina commercial plate yaani plate namba nyeupe na sio ya njano.

LESENI YA LATRA

Latra ni kifupi cha Land Transport Regulatory Agency. Hii ni Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini na ndio inayotoa leseni za barabarani au road licence ambayo inahitajika ili kuweza kuendesha gari Uber.

Mmiliki wa gari unaweza kujiandikisha kupata leseni hii kwa kuwatembelea ofisi zao zilizopo Plot 57 Serengeti Road, Mikocheni, Dar es Salaam .Au unaweza kutuma maombi kupitia website yao HAPA

CHETI CHA TABIA NJEMA

Hii ni Police clearance report ambayo unaweza kuifata kwenye kituo chako cha karibu. Lengo kuu ni kuhakikisha usalama wa abiria wa Uber kwa kutoajiri madereva wenye historia ya uhalifu.

Kama wewe ni raia mwema ambaye haujawahi kupata misukosuko yoyote na polisi basi utaweza kupata cheti hiki kwa urahisi na kuendelea na maombi.

B. JISAJILI KUWA DEREVA UBER KUPITIA WEBSITE YA UBER.

Unahitaji anwani ya barua pepe au email address pamoja na simi janja (smartphone) yako tu kuanza zoezi hili la usaili.

Bonyeza hapa ili upelekwe moja kwa moja kwenye website ya Uber Tanzania ya Kiswahili. Kisha bonyeza kitufe kilichoandikwa “Jisajili ili uendeshe gari”.

jisajilii kuwa dereva Uber ufanikiwe

Hatua ya kujiandikisha kuwa dereva wa Uber imegawanywa katika sehemu tofauti kama inavyoonekana kwenye picha zinakazofuata.

Sehemu ya kwanza ni kusajili taarifa zako muhimu kama inavyoonekana kwenye picha inayofuata.

jinsi ya ku jissajili kuwa dereva uber
Fomu ya uber

Kisha unashauriwa kupita mafunzo mafupi (Virtual info session) ya vitu muhimu unavyopaswa kuvifahamu kama dereva wa Uber. Mfano ni jinsi ya kutumia app, jinsi bei zinavyohesabiwa, jinsi ya kuwasiliana na abiria na mengine mengi.

Jinsi ya kutengeneza pesa kupitia Uber

Kwa hiyo ni muhimu sana kuanza kwa kupitia mafunzo kwanza ndipo uelendelee na usajili.

Sehemu zinazofata ni rahisi tu ambapo ukibonyeza utaambiwa upige picha document zako kwa mfano leseni, bima, road licence ya LATRA nk.

nyaraka za kujisajili kuwa dereva uber

Mwisho kabisa kuna survey au tafiti ambapo ukibonyeza utaweza kuchagua lugha ya Kiswahili (au kiingereza) na utapewa maswali ambayo unatakiwa kuyajibu ili kufahamu kama unafaa kuwa dereva wa Uber.

Chagua wakati ambao upo sehemu yenye utulivu na muda wa kutosha ili ujibu kwa ufanisi zaidi. Kutoa majibu ambayo si sahihi kunaweza kukuharibia nafasi yako ya kuruhusiwa kuendesha abiria Uber.

vigezo vya kusajiliwa uber

Baada ya kumaliza hatua hii na kutuma document zote unatakiwa kusubiri kwa masaa au siku kadhaa ili ombi lako likaguliwe na upate ruhusa ya kuanza kuendesha abiria na kutengeneza pesa kupitia jukwaa la Uber.

Jisajili kuwa dereva Uber na ujiajiri.

Kwa kifupi, mtu yoyote mwenye vigezo vilivyozungumziwa katika makala hii anaweza kukubaliwa kuendesha Uber. Cha muhimu ni kuandaa nyaraka zote kabla ya kuanza hatua ya kujisajili, kuhakikisha nyaraka ni up-to-date na picha unazopiga zionekane vizuri.

Pia hakikisha unajibu maswali vizuri katika kile kipengele cha mwisho cha tafiti.

5 thoughts on “JISAJILI KUWA DEREVA UBER NA KUBALIWA HARAKA!”

  1. Pingback: JISAJILI KUWA DEREVA BOLT NA KUBALIWA CHAP CHAP!

  2. Pingback: MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER TANZANIA 2022.

  3. Pingback: KILA DEREVA UBER/BOLT LAZIMA AWE NA VIFAA HIVI

    1. Ndio Watson unaweza kujisajili. Pitia machapicho yetu kwenye tovuti yetu ili upate kujua jinsi ya kujisajili lakini pia unaweza kuwasiliana moja kwa moja na kampuni unayotaka kujiunga nayo ili wakupe msaada zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *