Bolt ni kampuni ya usafirishaji iliyoanzishwa nchini Estonia na kusambaa kwenye nchi mbalimbali duniani. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa Bolt ina wateja zaidi ya milioni 75 na madereva zaidi ya milioni 1.5 ambao wanatoa huduma za usafiri kwenye app ya Bolt.
Maelfu ya madereva wa Tanzania wameweza kujiajiri au kuajiriwa kuendesha vyombo vya usafiri Bolt na kutengeneza fedha ambazo hawakuwa wakitengeneza wakati wanaendesha taxi.bajaji, boda boda za kawaida au madaladala.
Hii ni kwasababu dunia inabadilika na teknolojia inakua kwa kasi sana hivyo watu wengi zaidi wanapenda wepesi wa kupata usafiri kupitia simu zao.
Ndani ya makala hii utazifahamu njia sahihi za kujisajili kuwa dereva Bolt pamoja na nyaraka zote unazotakiwa kuwa nazo ili kuhakikisha ombi lako linakubaliwa bila vikwazo.
Jisajili kuwa dereva wa Bolt Tanzania

Kabla ya kuanza harakati za kujisajili kama dereva jiulize maswali yafuatayo :
- Je una umri sahihi wa kuendesha vyombo vya usafiri?
- Una leseni ya kuendesha chombo cha usafiri?
- Huduma za Bolt zinapatikana kwenye mji uliopo?
- Unamiliki chombo cha usafiri?
Baada ya kujitathmini anza na mchakato wa kujisajili ili uanze kuendesha mapema iwezekanavyo kwa kufata hatua zifuatazo.
A. ANDAA NYARAKA ZINAZOHITAJIKA
Ili kuweza kukubaliwa kuendesha abiria Bolt unahitaji kuwa na nyaraka zifuatazo.
- Leseni ya udereva wa magari ya Class C2 au C3, A1 ya pikipiki(boda) au A3 ya bajaji.
- Picha ya dereva
- Picha ya chombo cha usafiri
- Bima ya gari commercial (ya biashara)
- Kadi ya gari la shughuli za biashara.
- LATRA road licence
- Hati ya tabia njema kutoka Polisi.
AINA SAHIHI YA LESENI
Tanzania ina makundi 8 ya leseni za udereva ambayo A,B,C,D,E,F,G na H. Kundi A ni leseni za kuendesha pikipiki za aina tofauti (A1, A2, na A3). Kundi B ni leseni za vyombo binafsi vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa, magari ya biashara na magari ya kutoa huduma kwa umma.
Ili kuendesha piki piki (Boda) au bajaji Bolt unatakiwa kuwa na leseni ya Class A1 (Boda) au A2 (Bajaji) na Class C2 au C3 kwa dereva wa magari.
Leseni Class C2 ni Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 15 lakini wasiozidi 30 pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
Leseni Class C3 ni leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 4 au pungufu akiwemo dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
Leseni Class D ni leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma. Hii ndio ya kuendesha magari madogo ya mizigo ya biashara.
Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu uchambuzi wa makundi ya leseni.
Kumbuka unaweza kubadilisha leseni yako kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). Kisha jisajili kuwa dereva Bolt na wewe uweze kutengeneza kipato kikubwa kutokana na ujuzi wako.
Fahamu hatua zote za kubadili leseni yako kuwa Class C pamoja na gharama zake.
KITAMBULISHO CHA DEREVA
Ili ku jisajili kujisajili kuwa dereva Bolt ni lazima kuwa na moja ya vitambulisho vifuatavyo:
- Kitambulisho cha utaifa NIDA
- Kitambulisho cha mpiga kura
- Passport ya kusafiria
- Cheti cha kuzaliwa
PICHA YA DEREVA
Simama katikati ya camera, hakikisha kuna mwanga wa kutosha na hakuna vitu vyovyote nyuma yako zaidi ya ukuta au kitambaa cheupe. Picha ioneshe vizuri uso mzima hadi mabega, usivae miwani ya jua wala usitumie picha ya kwenye leseni.
PICHA YA CHOMBO CHA USAFIRI
Kama wewe ni dereva piki piki, bajaji au gari unatakiwa kuwa na picha nzuri ya chombo chako. Hakikisha chombo ni kisafi, picha ina mwanga mzuri na plate namba inaonekana na kusomeka kirahisi.
BIMA YA GARI
Bima ya magari ya binafsi na magari ya biashara ni tofauti. Hakikisha gari lako au la mwajiri wako limekatiwa bima ya biashara ambayo haijaisha muda wake.
KADI YA GARI LA ABIRIA
Ili gari likubaliwe kuendesha abiria wa Bolt ni lazima liwe na kadi ambayo inaonesha matumizi yake ni ya biashara na lina commercial plate yaani plate number nyeupe na sio ya njano.
LESENI YA LATRA
Kama tulivyoeleza katika makala ya jinsi ya kujisajili Uber, Road Licence ya LATRA inahitajika pia ili kuweza kuendesha gari Bolt.
Mmiliki wa chombo unaweza kujiandikisha kupata leseni hii kwa kuwatembelea ofisi zao zilizopo Plot 57, Serengeti Road, Mikocheni, Dar es Salaam . Au unaweza kutuma maombi kupitia website yao HAPA
HATI YA TABIA NJEMA
Hii ni Police clearance report ambayo unaweza kuifata kwenye kituo cha Polisi cha karibu. Lengo kuu ni kuhakikisha usalama wa abiria wa Bolt kwa kutoajiri madereva wenye historia ya uhalifu.
B. JISAJILI KUWA DEREVA WA BOLT KUPITIA WEBSITE YAO.
Unachohitaji ni anwani ya barua pepe au email address pamoja na namba ya simu ya smartphone yako tu kuanza zoezi hili la usaili. Hatua ya kwanza ni kubonyeza hapa ili upelekwe moja kwa moja kwenye website ya Bolt Tanzania ya Kiswahili. Kisha uanze kujisajili.

Kama una usafiri zaidi ya mmoja na umeajiri madereva hakikisha unabonyeza maneno ya kijani kujisajili kwa njia tofauti kidogo.
Taarifa binafsi na za chombo cha usafiri
Hatua inayofata ni kuingiza taarifa chache kuhusu wewe na chombo cha usafiri unachapanga kutumia kuendeshea abiria. Taarifa hizi ni majina yako mawili, lugha unayopendelea kutumia pia namba ya simu ya dereva wa Bolt aliyekujulisha kuhusu Bolt kama yupo.
Kama hakuna mtu aliyekurefer Bolt acha sehemu hii wazi.

Taarifa za gari za kujaza ni Aina ya gari(Mfano TOYOTA), Model (mfano IST), mwaka gari lilipotengenezwa, namba ya gari na rangi.

Picha za nyaraka.
Hatua inayofuata ni kupiga picha nzuri za nyaraka tulizozichambua hapo juu kisha kuzi upload kwenye sehemu husika.
Kila nyaraka yenye expiry date hakikisha unajaza ili hatua hii iweze kukamilika na uweze kuendelea na hatua ya mwisho ya kusubiri ombi lako likaguliwe na upate majibu kama umekubaliwa.


Mchakato huu wa kujisajili kuwa dereva wa Bolt utaenda haraka zaidi kama utafata mtiririko huu na kuandaa kila kitu kabla ya kuanza. Pia kwa kuchagua siku nzuri na sehemu nzuri iliyotulia ili uweze kujaza fomu kwa umakini zaidi.
Tunatumaini makala hii itakusaidia katika mchakato wako wa kuwahi fursa hii. Tafadhali share na watu wengine ambao wanatamani kuanza biashara hii ya kuendesha abiria Bolt.
Karibu Weibak uweze kupata mbinu nzuri sana za kutengeneza kipato kikubwa zaidi kwenye majukwaa ya usafiri kama Bolt, Uber nk.
Pingback: MAGARI YANAYOKUBALIWA KUSAJILIWA UBER TANZANIA 2022.
Ahsante kwa makala hii. Je, hii process inachukua muda gani yangu kuapply mtandaoni mpaka kuanza kazi?