Je, dereva unajihisi kunyonywa na majukwaa ya teksi mtandao?

Moja ya maoni ambayo tumeyapokea kwa wingi kutoka kwa wasomaji wetu katika machapisho yaliyopita, ni jinsi ambavyo madereva wanajihisi kunyonywa na majukwaa ya teksi mtandao kwa madai kuwa majukwaa hayo yamekuwa yakiwakata ada kubwa kwa kutumia huduma zao. Na wengine wakaenda mbali zaidi kwa kudai kuwapelekea kupata hasara. Yaani pesa wanayowekeza katika biashara hii ni kubwa kuliko kile wanachokiingiza kama faida.

Kutokana na hayo, timu ya Weibak Carsharing imefanya mazungumzo na Editha Deus Batumbe, mama ayefanya shughuli za usafirishaji wa abiria kwa kutumia majukwaa ya teksi mtandao kama Bolt na Paisha.

Kama dereva, Editha anaeleza sababu iliyomsukuma kuanza kujishughulisha na usafirishaji wa abiria kupitia majukwaa ya teksi mtandao, changamoto anazokumbana nazo na mbinu anazotumia kuepukana na changamoto hizo.

Sikiliza Mahojiano yote hapa 

3 thoughts on “Je, dereva unajihisi kunyonywa na majukwaa ya teksi mtandao?”

  1. Bolt Wanakata Asilimia 23 imagine hapo Kama Dereva Unavyoumia Wakati Mwingine tunafanya Kazi ilimradi Siku Ziende tu na Sio Kwa Ajili Ya Kutengeneza Future Za Maisha Yetu na Familia Zetu bali Tunawatengenezea Wajuaji future Zao Waendelee kuwa Na Maisha Mazuri inasikitisha Lakini hatuna Jinsi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *