akaunti ya dereva uber tanzania kufungwa

FUNGUA AKAUNTI YA UBER ILIYOFUNGWA KWA KUFATA NJIA HIZI

Katika makala iliyopita uliona ni jinsi gani akaunti yako ya dereva inaweza kufungiwa na Uber na kukuzuia kufanya kazi na kutengeneza pesa. Katika makala hii tunaenda kukuonesha jinsi ya ku fungua akaunti ya Uber iliyofungwa na kuzuia kufungiwa tena.

Je umefungiwa akaunti yako ya dereva Uber?

Usivunjike moyo, hili janga huwa linawatokea madereva wengi tu tena hata zaidi ya mara moja katika shughuli zao za kutafuta kipato kwenye majukwaa haya.

Unapofungiwa akaunti si mara zote ina maanisha wewe una makosa, inawezekana ukafungiwa kimakosa tu kwasababu mwisho wa siku teknolojia zinaweza kupata hitilafu hata kama kampuni ni kubwa kiasi gani.

Unajuaje sababu za akaunti kufungwa?

Mara nyingi Uber huwa haiambatanishi sababu za kufungiwa akaunti kwenye ule ujumbe wa akaunti kufungwa.

Kama na wewe haujaelewa vizuri kwanini umefungiwa, basi tembelea ofisi zao uwaulize kinachoendelea.

Wakati mwingine unaweza kuingia kwenye app yako ya dereva na kukuta ujumbe kwenye screen kuwa akaunti yako inahitaji attention yako.

 • Panapotokea ujumbe kama huu utaona na kitufe cha kuwasiliana na huduma kwa wateja kinachosema “Contact Support” ambacho unatakiwa kubonyeza.
 • Itakuja fomu ya kutuma kwa muhudumu wa customer care. Uliza kwanini akaunti yako imefungwa na hatua gani zinatakiwa kuchukuliwa ku fungua akaunti ya Uber iliyofungwa kutokana na tatizo lako.
 • Kama kipengele hiki hakipo ni bora kwenda tu moja kwa moja kuwauliza ofisini au kuwapigia simu kama upo nje ya Dar es salaam.

Ukienda kupata suluhisho kwa wahusika kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa hata kama kosa kweli ulikuwa nalo. Lakini pia yapo makosa ambayo kama ni kweli umeyafanya hauwezi ku fungua akaunti ya Uber na kuendelea kuendesha abiria tena.

Makosa haya ni kama yafuatayo:

1. Kujeruhi abiria au kumtishia usalama wake.

Kwa kampuni kubwa kama Uber abiria akijeruhiwa na dereva kwa njia yoyote ambayo si ajali lazima dereva afungiwe akaunti. Hii ni kwasababu:

kwanza taarifa ikisambaa kampuni itapoteza abiria wengi kutokana na hofu hivyo kushusha kipato.

Pili abiria anaweza kuipeleka kampuni mahakamani na kudai fidia kwasababu Uber imempa fursa mtoa huduma ambaye ni hatari kwa watu wengine. Mara nyingi sana hili likitokea kampuni huishia kulazimika kumlipa mlalamikaji.

Tatu ukijeruhi mtu na akatoa taarifa polisi tayari kile cheti cha polisi cha tabia bora inabidi unyang’anywe kwasababu hilo ni kosa la jinai.

2. Unyanyasaji wa kijinsia

Hii inajumuisha tendo lolote analofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono. Unyanyasaji huu hutokea zaidi dhidi ya wanawake ingawa wanaume pia wanaweza kufanyiwa.

Ukatili wa kijinsia hujumuisha ukatili wa kingono kama kushikwa sehemu za mwili bila ridhaa na kubakwa. Pale abiria anapotoa malalamiko ya kufanyiwa vitendo hivi ni lazima dereva afungiwe akaunti na kesi ifunguliwe polisi.

3.Uhalifu wakati ukiwa online

Shughuli za uhalifu kama kuibia abiria au kusafirisha wahalifu wanaoenda kufanya tukio ambalo unafahamu kuwa wanaenda kulifanya hazisameheki Uber. Pia utapeli wa kurefusha safari au ku hack jukwaa la Uber huweza kupelekea akaunti ifungwe milele.

4. Nyaraka feki

Hii hupelekea kufungwa akaunti moja kwa moja kwasababu dereva anaonekana mtu wa hatari, na pia kwasababu hili pia ni kosa kutokana na sheria za nchi, dereva anaweza kufunguliwa kesi. Uber hairuhusu madereva wenye historia ya kufunguliwa kesi au kufungwa jela, kwa hiyo automatically hautaweza tena kufungua akaunti ya Uber iliyofungwa kwa chanzo hiki.

Kama una uhakika kuwa haukustahili kufungiwa akaunti au kama umekubali kosa na unataka kuendelea na kazi unaweza.

FUNGUA AKAUNTI YA UBER ILIYOFUNGWA KWA KUFATA HATUA HIZI

1. Nenda kwenye ofisi za Uber

Mara baada ya kufunguwa akaunti weka muda uende mwenyewe kwenye ofisi za Uber na ukawaelezee tatizo lako. Mara nyingi wao wanaweza kukusaidia kurudisha akaunti yako haraka hasa kama ulifungiwa kimakosa, au kama una vithibitisho kuwa hauna hatia ya kosa walilokufungia.

Kama upo Dar es salaam tazama HAPA ili kupata direction za ofisi zote mbili za Uber na ujue ipi ipo wazi kutoa huduma. Kama upo nje ya Dar basi kwenye link hiyo hiyo utakuta namba za simu pamoja na njia nyingine za kuwasiliana na uongozi wa Uber.

Hakikisha unapofika ofisini uwe umejiandaa kwa kiasi kikubwa kutoa maelekezo na vithibitisho vyako. Kwa kukushauri tu ni kwamba uwe mtulivu na usikasirike kirahisi pale ambapo hautapata huduma uliyokuwa unaitegemea.

Kwa kawaida walalamikaji ni wengi, hufika pale wakiwa tayari wamekwazwa kutokana na kufungiwa akaunti. Na wahudumu nao mara nyingi huwa wamehudumia walalamikaji wengi na hivyo wao pia huchoka na kukwazwa na hasira za wadau.

Kwa hiyo usipopata majibu ya kuridhisha endelea kuwa mpole na kurudi wakati mwingine ukiwa umejipanga zaidi au ukipata nyaraka kamili wanazotaka uwaoneshe.

2. Update nyaraka

Kama vile akaunti yako imefungwa kwasababu nyaraka zako kama leseni na bima zimekwisha muda wake hatua ya ku fungua akaunti ya Uber iliyofungwa inakuwa rahisi tu.

 • Hakikisha unalipia bima na unapata leseni mpya.
 • Sign in kwenye tovuti ya Uber.
 • Kisha binyeza “My Profile”
 • Halafu bonyeza “Manage Documents”
 • Hapa unaweza kupakua nyaraka mpya

3. Kamilisha kozi ya kuboresha viwango

Kama vile akaunti yako imefungwa kwasababu ya alama ya nyota kushuka chini ya 4.6 basi unaweza kufunguliwa akaunti kama utaweza kufanya kozi maalumu ya kuinua viwango.

Kampuni ya 7×7 Experience inatoa kozi hii online kwa ajili ya madereva wote waliofungiwa akaunti kwa tsh 113,355/= tu. Unapomaliza kozi unachotakiwa ni kutuma cheti kwa uongozi wa Uber au kukichapisha na kukipeleka ofisini kwao.

Baada ya kukipitia akaunti yako itarudishwa hewani kwasababu utaonekana kuwa umepata elimu inayofaa ya kukusaidia kutoa huduma bora na kuepuka kupewa alama za chini na abiria.

JINSI YA KUEPUKA KUFUNGIWA AKAUNTI YA DEREVA UBER

 1. Endesha kwa umakini: heshimu sheria za barabarani na usiendeshe ukiwa umetumia kilevi cha aina yoyote ile.
 2. Endesha mara kwa mara: Usikae muda mrefu sana bila kuendesha kabisa. Jipangie masaa machache uendeshe hata kwa lisaa limoja kuliko kutoendesha kabisa. Epuka pia ku cancel safari mara kwa mara.
 3. Kuwa mstaarabu: Madereva wengi hufungiwa akaunti kwasababu abiria wanawaripoti tabia zisizowafurahisha. Kumbuka wewe ni mtoa huduma professional na abiria ni mfalme. Hata unapokosewa heshima vumilia na uendelee na kazi kwa ustaarabu.
 4. Pata alama za juu: Soma hapa jinsi ya kupata alama ya 5 stars nyingi ili kuhakikisha haufungiwi akaunti kutokana na alama ndogo.
 5. Update nyaraka mapema: Usichelewe ku renew leseni na kulipia bima ya gari. Wahi ili kuepuka akaunti yako kufungiwa.
 6. Usivunje sheria: Kama utapata lalamiko lolote katika sehemu nyingine ya maisha yako ambalo litakalorekodiwa kwenye kituo cha polisi basi lazima akaunti ya ko ifungwe. Uber haitaki dereva yoyote mwenye historia na vyombo vya usalama.

Je, umewahi kufanikiwa ku fungua akaunti ya Uber ambayo ilifungwa? Mchakato wake uliuonaje? Tushirikishe kwenye sehemu ya comments ili madereva wengine waweze kupata elimu kutoka kwako.

2 thoughts on “FUNGUA AKAUNTI YA UBER ILIYOFUNGWA KWA KUFATA NJIA HIZI”

 1. Nyinyi ni wapumbavu Sana maana mnaaribu mageri yetu na kutufungia huduma kwa sabubu ya awateja wa kadi sasa mnataka pesa za kufungua huduma kiasi cha pesa hicho cha 113355 za nini tena na hiyo ni huduma za kimtaifa huo ni utapeli..

 2. Lusajano David Ngulwa

  Please niliambiwa account yangu ilifungwa kwa kuwa nilikuwa nafanya ubabaidu ki ukweli sikujua haya mambo ya mitandao ndugu naomba radhi kwa yote ili nifunguliew account yangu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *