Kuongezeka kwa biashara za teksi mtandao kama vile Bolt, Paisha, InDriver, Littleride na kadhalika, kumebadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi watu wanavyosafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Katika chapisho hili tutaangazia faida na hasara za dereva kutumia huduma za teksi mtandao, na kwa nini ni muhimu kuendelea kutumia teksi mtandao?
Faida za kutumia teksi mtandao
Kuepusha dereva kumpotezea muda abiria: Kupitia teksi mtandao, dereva anaweza kutumia ramani kumfuata abiria punde tu anapokubali ‘request’ yake. Hii inamfanya dereva kwenda kwa wakati na kuepusha abiria kumsubiri kwa muda mrefu.
Kuwa na aina zaidi ya moja ya vyombo vya usafiri: Majukwaa ya teksi mtandao kama vile Bolt, Paisha, Ping na kadhalika, yanampa dereva fursa ya kutoa huduma ya usafiri kupitia aina mbalimbali za vyombo vya usafiri. Kuna magari, teksi na pikipiki. Aina tofauti zina bei tofauti.
Ufuatiliaji wa safari kwa uwazi: Majukwaa ya teksi mtandao yanatoa fursa kwa dereva na abiria wake kufuatilia safari kwa uwazi. Pindi tu dereva anapokubali kumsafirisha abiria, wote wanaweza kufuatilia mahali na njia wanayopita. Hii hutengeza mazingira salama na rafiki kwa dereva na abiria wake.
Abiria atalipa nauli kulingana na umbali uliomsafirisha: Hii humsaidia zaidi dereva kuepusha kulipwa kiwango cha chini ambacho kinaweza kupelekea hasara katika biashara yake.
Abiria kujenga uaminifu kwa dereva: Wamiliki wa majukwaa ya teksi mtandao huondoa madereva wasio na taaluma. Hiyo inategemeana na maoni ambayo abiria hutoa kwa kukadiria utendaji kazi wa dereva husika kupitia nyota. Ikiwa dereva atapata ukadiriaji wa chini mara kwa mara, jukwaa humwondosha dereva huyo na nafasi yake huchukuliwa na dereva mwingine. Ili kuepuka changamoto hii, madereva hufanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa hata kupelekea kuaminika miongoni mwa abiria wao.
SOMA ZAIDI: Changamoto za Uber, Bolt Fursa kwa Majukwaa Mengine ya Teksi Mtandao?
Hasara za kutumia teksi mtandao
Baadhi ya maeneo hayajasasishwa kwenye ramani: Hii hupelekea madereva kulazimika kuzunguka huku na kule kutafuta ‘location’ambayo abiria amekusudia kufika.
Teksi mtandao hutumiwa zaidi maeneo ya mjini: Dereva atalazimika kufanya kazi zaidi katika maeneo ya mjini na maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu hata kupelekea kuyatenga maeneo yaliyopo nje ya mji.
Ili kutumia huduma hii nchini, unahitaji ‘simcard’ ya Tanzania ili kusajili akaunti na pesa taslimu za kulipia. Bila shaka, unaweza kuhamisha, lakini ni lazima uwe na kadi ya benki iliyoidhinishwa nchini hususan ikiwa wewe sio raia wa Tanzania.
Wakati mwingine, kasi ya programu hizi kufanya kazi hushuka hasa pale kunapokuwa na watumiaji wengi kwa wakati mmoja.
Kwa nini dereva utumie teksi mtandao?
Watu wanapendelea kutumia teksi mtandao ili kuepuka changamoto mbalimbali ikiwemo msongamano wa magari, kuondokana na changamoto ya maegesho hasa katika miji mikubwa hivyo kufanya teksi mtandao kuwa suluhisho pekee kwenye changamoto hizi.
Majukwaa ya teksi mtandao yamekuwa kimbilio kwa wageni wengi hasa kutoka nje ya miji kutokana na kuwa na imani kuwa majukwaa haya ni salama na huwaepusha na ulaghai au kutozwa gharama za juu kwa usafiri.
Sasa madereva hawana haja ya kusubiri kwa muda mrefu katika stendi za mabasi au vituo vya daladala, badala yake, wanaweza kuunganishwa na abiria wao kupitia majukwaa ya teksi mtandao katika eneo lolote ambako wanapatikana.
Majukwaa ya teksi mtandao humruhusu dereva kufanya kazi wakati wowote, ni juu ya dereva kuchagua ni wakati gani anahitaji kuwasha programu ya teksi mtandao tayari kwa kupokea ‘requests’ za abiria wanaohitaji kusafiri.
Niongezee neno kiongozi kwenye asara za taksi mtandao
Madereva kutosikilizwa kwa wakati kwenye malalamiko ya kupandishiwa bei za trip au kushushwa bila dereva kutaharifiwa kwa wakati kingine kuyojali hii nei itakayo punguzwa kwa dereva itamfaa?
Asante sana Bruno tunashukuru kwa mchango wako.
Nafatilia sana nakala zako kiongozi unanijenga sana kiakili na uwelewa wangu unaongezeka katika kufanya kazi kwenye aya majukwaa na mambo mengine japo kuna changamoto za aya majukwaa kwa upande wa kujisajili utakuta magari yanaongezeka kwa wingi kwenye majukwaa ya kiwa na no za njano yani siyo ya kufanyia hii kazi ya taksi mtandao hila madereva wanao ziendesha unakuta wanafanya taxi mtandao pia kukodishana account hii ni hatari sana kiusalama kwa mtoaji na mpokeaji pia naomba upatapo mda utoe elimu kwa upande huu kiongozi asante sana
Tunafurahia sana mchango na mhitikio wa wadau kama wewe katika ufanyaji kazi wetu. Tutajitahidi kutoa elimu ya kutosha ili iendelee kuwa msaada kwenu.