Kutokana na taarifa zilizopo, changamoto za madereva Uber/Bolt ni nyingi ingawa madereva bado wanaendelea kutoa huduma. Watu wengi hudhani kuwa kwasababu kampuni ni kubwa inayotokea nchi maarufu kila kitu kitakuwa murua katika utenda kazi wake.
Lakini ukweli ni kwamba ingawa sekta hii ni ya kiteknolojia zaidi, bado madereva wanapitia mambo ambayo mara nyingi huwafanya kutamani kukata tamaa.
Lengo la makala hii sio kukukatisha tamaa auche kujisaajili au uache kuendesha abiria wa Uber. Lengo letu ni kuwaelimisha madereva wapya, wazoefu pamoja na wamiliki magari waliojiunga na wanaotaka kujiunga na fursa hii. Kwani kila fursa huja na changamoto zake na ni muhimu kuzitambua.
Ni muhimu kila mtu afahamu kwamba ndio kuna hela nyingi kwenye kuendesha abiria Uber/Bolt lakini pia kuna vikwazo ambavyo wanatakiwa kuwa tayari kuvishinda.
CHANGAMOTO ZA MADEREVA UBER/BOLT TANZANIA
Tumeamua kuzipanga changamoto hivi kwenye makundi makuu matatu kama ifuatavyo.
A. APP YA DEREVA
App mara nyingi inaweza kuacha kufanya kazi muda wowote ambao dereva anahitaji kuwa hewani apate abiria. Kwasababu teknolojia ni kitu kinachohitaji ufundi wa hali ya juu tatizo hili si rahisi kuepukika.
Matatizo ambayo yamekuwa yakiripotiwa zaidi na madereva ni kama yafuatayo.
1. APP KUGANDA
Application nyingi za simu huwa zinaganda hivyo kufanya kila kitu kushindikana hata kuzifunga app hizo. Tatizo hili linaweza kuwa linasababishwa na app ya kampuni au inaweza kuwa tatizo kwenye simu ya mtumiaji.
Kama simu yako ina Memory ndogo basi tatizo hili huwa linatokea mara nyingi zaidi ya wale ambao simu zao zina memory kubwa pamoja na RAM. App yako ya Uber/Bolt au nyingine ikiganda unaweza kuchukua hatua zifuatazo kuirudisha iendelee vizuri.
- Funga app na uiwashe tena
- Log out, subiri dakika mbili halafu log in tena
- Restart simu na ujaribu tena
- Delete app yako kisha ui-install tena
- Update app yako
Jinsi ya kuzuia app ya Uber/Bolt kuganda au ku-freeze.
- Kwanza hakikisha unafuta vitu ambavyo huvihitaji kwenye simu yako hasa apps nyingine ambazo huwa hauzitumii sana.
- Restart simu yako kabla ya kuanza shift yako ya kuendesha abiria.
- Restart simu yako kila ukimaliza kucheza game za simu: michezo ya kwenye simu huwa inatumia memory kubwa sana. Hakikisha hauna app nyingi za games.
- Update system ya simu: Unapopata ujumbe kuwa updates za simu yako zipo tayari basi update mara moja. Pia update app ya Uber kila baada ya update mpya kuwepo. Kila kitu kikiwa up-to-date kwenye simu yako tatizo la app kuganda litapungua sana.
- Reset simu: Kama simu yako imekuwa taratibu sana na inakwama kwama mara nyingi basi ifanyie factory reset na uanze upya.
- Upgrade simu: Inawezekana app zinaganda kwasababu ya ubora wa simu. Wekeza kwenye simu yenye uwezo mkubwa zaidi ili isilete shida.
2. HITILAFU ZA GPS
Location errors ni moja ya changamoto za madereva wa Uber/Bolt ambazo zinakera sana kwasababu zinaleta matatizo kwenye kupata malipo halali ya safari.
Kama umewahi kupata tatizo hili basi inawezekana pia kuwa simu yako ina tatizo la gps. Hii ni issue huwapata madereva wengi bila kujali wanatumia simu za Android au ios.
Hakikisha location ya simu yako ipo on kupitia setting zake. Kama unatumia simu android hakikisha settings zako za location ziwe on kwenye “High accuracy”.
Ufanye nini app ya dereva ikigoma kufanya kazi?
- Jaribu kuwasiliana na madereva wengine kuwauliza kama na wao wanatatizo hili
- Wasiliana na Uber/Bolt hasa kwenye mitandao ya jamii uwataarifu kuhusu tatizo.
- Kuwa na backup plan: washa app ja majukwaa mengine na uendeshe abiria wao. Ukiwa na mbadala hautakuja kuumiza kichwa pale ambapo jukwaa moja litapata hitlafu.
SOMA: Jinsi ya kujisajili kuendesha abiria wa Bolt.https://weibakcarsharing.com/?p=619
B. CHANGAMOTO ZA KAMPUNI
Siku zote lengo kuu la biashara ni kutengeneza faida. Makampuni yaliyotengeneza majukwaa haya ya usafiri kama Uber na Bolt nayo huhitaji kutengeneza kipato kikubwa. Kwa hiyo mara nyingi kuna hatua na sheria wanazochukua ambazo zinaumiza madereva huku wao zikiwapunguzia hasara.
Madereva wengi wamekuwa wakilalamika hadi kufikia hatua ya kuamua kufanya mgomo kutokana na matatizo yafuatayo.
3. MAPATO
Hadi hivi karibuni kumekuwa na tetesi ya madereva Uber na Bolt kufanya mgomo kutokana na makato ya kipato. Kwasababu kampuni zinataka faida, madereva wamekuwa wakikatwa 20% hadi 30% ya mapato ya safari .
Hii inasababisha madereva kupata faida ndogo zaidi na kuwakatisha tamaa.
4. BEI NDOGO
Mojawapo ya changamoto za madereva Uber/Bolt ni bei ya nauli. Hadi sasa abiria hulipia tsh 450 tu kwa kila Kilomita moja. Hii ni nafuu kwa abiria lakini kwa madereza ni ndogo sana hasa ukuzingatia kwamba wanakatwa 20% hadi 30% ya nauli.
5. ACCOUNT KUFUNGWA
Makampuni kama Uber na Bolt yamekuwa mepesi kufungia akaunti za madereva kabla ya kusikiliza malalamiko yao vizuri hata pale ambapo abiria ndiye mwenye kosa.
Juu ya hapo si rahisi hasa kwa Uber kupata mtu wa customer care wa kusikiliza malalamiko na kuyatatua haraka.
SOMA: Jinsi ya kuwasiliana na uongozi wa Uber ili kutatuliwa tatizo lako mapema.
6. KUTOLIPWA FIDIA
Madereva wanatakiwa kulipwa fidia na makampuni husika pale wanapofata wateja mbali na pick up point. Lakini imekuwa ikitokea kuwa madereva wengine wamekuwa wakifata abiria wengi hadi Kilomita mbili na zaidi huku wakijua watalipwa na wasilipwe kabisa.
C. ABIRIA
Madereva wengi wamekuwa wakilalamika sana kuhusu abiria. Hiki ni kitu cha kukitegemea lakini unapofikiria kuwa ni kitu ambacho kinaweza kutokea mara nyingi kila siku unaweza kupoteza mori ya kufanya kazi.
Changamoto ambazo abiria huwapa madereva ni kama zifuatazo:
7. KUTOJUA KUTUMIA APP
Abiria wengi hasa wapya huwa hawafahamu kutumia huduma hii ya kusafirishwa hivyo husababisha kupoteza muda na pesa kwa madereva.
Moja ya changamoto kubwa ni abiria kutojua kusoma gps na kuingiza taarifa sahihi za eneo walilopo wanapotaka kufatwa na dereva. Hii huweza kupelekea dereva kusimama sehemu ambayo ni mbali na abiria alipo hivyo kusababisha kupoteza muda mwingi sana kumtafuta na kumpata.
8. KUTOKUA TAYARI

Kuna tatizo kubwa la abiria kuitisha gari kabla ya kumaliza kujiandaa wakidhani kuwa wanaokoa muda. Hii husababisha dereva kuishia kumsubiri mtu nje kwa muda mrefu kwasababu labda hakukuwa na foleni na amefika haraka.
9. LAWAMA ZA KUCHELEWA
Kama tunavyofahamu, barabara za mjini huwa hazitabiriki kutokana na foleni na matengenezo ya muda mrefu. App kama za Uber/Bolt nk hujaribu kukisia muda ambao utatumika kumtoa abiria kutoka sehemu moja au nyingine. Lakini njia hii huwa sahihi kwa bara bara za nchi zilizoendelea tu.
Ingawa wengi tulinalifahamu hili, bado kuna abiria wengi hulalamikia madereva kwa kuchelewa kufika location zao. Wapo wengine wanaweza kumpa dereva alama ndogo kwasababu tu wameona kama wamechelewa wakati dereva hawezi ku-control foleni.
10. FUJO
Abiria ambao wametoka sehemu za starehe na kunywa pombe wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanya safari iwe ngumu. Ugumu huu unajumuisha harufu, kelele, matusi, kutotulia kwenye gari hadi kupigwa.
11. MAELEKEZO YA KUPITILIZA
Abiria huwa wanasahau kwamba baada ya safari kuanza na kuweka anwani ya location anapoelekea, barabara nzima inakuwa inaonekana kwenye app hivyo madereva wanajua jinsi ya kufika.
Baadhi ya madereva Uber/Bolt wamekuwa wakilalamika tatizo la abiria kutaka kubadilisha njia, kushushwa sehemu ambazo haziruhusiwi na hata kutoa maelekezo wakati yanaonekana kwenye gps.
12. MIZIGO
Madereva wengi wamekutana na abiria wengi ambao wana mizigo mikubwa sana na wanataka kusafirishwa kwa nauli ile ile ya mtu mmoja.
Hii inaleta kero kwanza ya kusaidia kupakiza, kupoteza muda, gari zito zaidi linatumia mafuta zaidi na pia ubora na usafi wa gari unaweza kuathiriwa na mizigo hiyo.
CHANGAMOTO ZINGINE ZA MADEREVA KWENYE MAJUKWAA YA USAFIRI WA KUSHIRIKIANA
13. USALAMA
Baadhi yamedereva wameripoti kupata changamoto hii hasa wakati wa kuendesha usiku. Ukweli ni kwamba wakati wa kuendesha watu kwenye majukwaa haya hauwezi kujua unabeba watu wa aina gani.
Ingawa kampuni kama Uber wana kampuni ya usalama ambayo madereva wanaweza kupiga simu na kusaidiwa, bado hofu ni kubwa na uwezekano wa kudhurika upo.
Hizo ndizo baadhi ya changamoto zinazolalamikiwa sana na madereva wa Uber na Bolt Tanzania.
Kuna changamoto nyingine ambayo umeipata na hatujaichambua? Tushirikishe kwenye sehemu ya komenti ili tujifunze kutoka kwako.
Pingback: JINSI YA KUTENGENEZA PESA NYINGI KWENYE UBER/BOLT %
Kuna baadhi ya app za madereva ambazo zinaonyesha Earning, Driver score, nk ila shida ni abiria akicancel na driver score inapungua
Asante Valentine kwa kutushirikisha kwenye changamoto hii uliyokumbana nayo.
Dereva kuazibiwa kwa kosa la mteja.
Abiria anafanya ombi la safar na dereva a nakubali lakini ndani ya sekunde 30 Abiria anaghali safar apo dereva anashushiwa kiwango cha ufanyaji kazi kwa kosa sio lake
Asante Donard kwa kutushirikisha kwenye changamoto hii uliyokumbana nayo.
Makato kwangu ndo changamoto jamani kwasabab huwez kumkata dereva 30% na ukiangalia karbia 90% ya uwekezaji kweny usafirishaji wa abiria ni juu yake Kuanzia gari/bajaj/piki piki….Haya vibali vyote juu yako,Service,parking ndo shida siku hizi ukiegesha sehemu kupakia mteja washa ku scan……Ukiwa unashusha wanaku scan….Yan unjikuta trip ya elfu 3 ushatumia elf 1 kwa ajili ya parking bado makato kwahyo unajikuta kwenye trip ya elf 3 umepata elf 1 Sasa kweli tutafika?…..
Pingback: MADEREVA UBER WENGI WANAACHA KAZI KWA SABABU HIZI. -