Bima ya ajali bure kwa madereva Uber

BIMA YA AJALI BURE KWA MADEREVA UBER WOTE TANZANIA

Ajali ni tatizo ambalo linaweza kutokea muda wowote na kukusababishia majanga na upungufu wa kipato. Ingawa madereva wote wanatakiwa kuwa na bima ya biashara ili kukubaliwa kuendesha Uber, bado kampuni ya Uber inakata bima ya ajali bure kwa madereva wake wote ili kuhakikisha wanapata maslahi yakutosha pale inapotokea ajali.

BIMA YA AJALI BURE KUTOKA BRITAM

Kuanzia tarehe 21/ 12 / 2018 kampuni ya Uber iliingia ubia na kampuni ya bima ya Britam kwa ajili ya kuwezesha bima ya ajali kwa ajili ya madereva pamoja na abiria wa jukwa hili.

SIFA ZA BIMA

Gharama za matibabu: Kama ajali itatokea ukiwa safarini, bima hii itakurejeshea gharama zote za matibabu ulizolipa baada ya ajali (Kuona daktari, X-Ray, dawa) ilimradi gharama hiyo isipite kima kilichowekwa.

Malipo ya kifo na mazishi: Ikitokea kwamba dereva amepoteza maisha kwa sababu ya ajali akiwa safarini, familia yake au warithi wake watapokea malipo kwa mkupuo mmoja.

Malipo ya Ulemavu wa Kudumu: Ikiwa kwa bahati mbaya utapata ulemavu kwa sababu ya ajali iliyotokea ukiwa unaendesha abiria wa Uber, utapokea malipo kwa mkupuo mmoja.

Kiasi cha malipo kitategemea kiwango cha ulemavu ulioupata , jinsi ilivyobainishwa na Britam.

Manufaa ya Malipo ya Kila Siku (majeraha): Kama utalazwa kwa zaidi ya siku 1 kutokana na ajali iliyotokea ukiwa kazini na baada ya hapo usiweze kufanya kazi kwa sababu ya majeraha hayo, utapokea malipo ya kila siku hadi daktari adhihirishe kuwa afya yako inaruhusu kuendelea na kazi.

Malipo haya ya kila siku yana kikomo cha siku 30.

Malipo ya Usumbufu: Kama Dereva atapata Jeraha la Mwili kutokana na ajali akiwa safarini, na kusababisha kulazwa hospitali kwa muda usiopoungua siku 1 atalipwa malipo kamili ya bima.

Manufaa haya yote yaliyotajwa yanapatikana tu katika hali zilizothibitishwa na daktari. Uber inaweza kubadilisha masharti haya kwa hiari yake.

KIASI CHA MALIPO YA BIMA

Bima ya ajali bure kwa madereva Uber itatolewa kama dereva atapata ajali akiwa safarini na akapata matatizo yafuatayo

Bima Masharti ya malipo
Bima ya matibabuHadi: 1,250,000 | Ambulensi hadi 500,000/=
Malipo ya kifo na matangaKifo: 5,000,000 tsh | Matanga :500,000/=tsh
Malipo ya ulemavu wa kudumuhadi 5,000,000/= tsh
Malipo ya kila siku (kwa majeraha100,000/= kwa siku
Malipo ya usumbufu (majeraha)50,000/= tsh

BIMA YA MAJERAHA SI SAWA NA BIMA YA GARI

Watu wengi huchanganya hizi bima mbili tofauti. Kila dereva Uber lazima awe anaendesha gari lenye bima ya biashara.

Bima ya ajali bure kutoka Britam ni nyongeza tu ya huduma ya Uber ili kusaidia kuongezea msaada pale dereva atakapopata matatizo akiwa kazini.

Ni wewe utaamua kuingia katika mpango huu wa bima. Unaruhusiwa kuikataa wakati wowote na hutaathirika kwa namna yoyote ile. Ukikataa, hutalindwa tena na Bima ya Majeraha kwa madereva inayojumuisha usaidizi wa gharama za matibabu na kupoteza fursa za mapato endapo utapata ajali ukiwa katika safari ya Uber.

Ikiwa una hakika kwamba hutaki ulinzi unaotolewa na Bima ya Majeraha kwa Washirika & Wasafiri, bonyeza hapa ili uweke maelezo yako na uwasilishe ombi la kuikataa, au tembelea Kituo cha Madereva wa Uber kilicho karibu nawe.

DEREVA ANAJISAJILI VIPI KUPATA BIMA YA AJALI BURE YA UBER?

Huhitaji kufanya jambo lolote kujisajili kwenye huduma hii. Kuanzia tarehe 21 Disemba 2018 una bima inayojali masilahi yako unapotumia programu ya Uber safarini.

Jinsi ya kujisajili kuendesha Uber 2022

Pia kumbuka bima hii inatumika hospitalini pale tu utakapopata ajali ya kazini na sio wakati unapoumwa tu. Lakini bado Uber imejikita katika kusaidia madereva kupata huduma hii bei nafuu kwa kupitia kampuni hii hii ya Britam.

VIGEZO VYA KUPATA FIDIA BAADA YA AJALI

UKIWA OFFLINE

Kama umepata ajali wakati haupo online kwenye app yako ya Uber basi bima hii ya Britam haiwezi kukupa malipo yoyote. Badala yake ile bima yako ya gari ndio itakuwa na jukumu hilo.

WAKATI UPO ONLINE LAKINI HAUNA ABIRIA

Bima ya Uber/Britam itakupa fidia kama umepata ajali wakati app yako ipo online hata kama hauna mteja unayemsafirisha. Hii ni kwasababu unapokuwa online ni kama upo kazini kwa hiyo inahesabika kama ajali kazini.

Uber itatoa fidia kwa athari hadi ulizosababisha wewe kwa dereva mwingine au gari lake pale ambapo bima yako ya gari haitalipia.

WAKATI UNA ABIRIA KWENYE GARI

Bima ya Uber ya Britam itafidia fedha nyingi zaidi kwa ajali zote pale unapokuwa na abiria kuliko ukiwa tu online peke yako bila abiria.

Kama wewe sio mwenye kosa au kama mwenye kosa kakimbia au bima yake haiwezi kukulipia gharama zako zote bima ya ajali ya Uber itakusaidia sana.

Ingawa Uber inatoa Bima ya ajali bure, unatakiwa kuhakikisha kuwa ile kampuni uliyokata bima ya biashara inafahamu kwamba unatumia gari lako kuendesha abiria kwenye majukwaa kama Uber.

HATUA ZA KUPATA FIDIA BAADA YA KUPATA AJALI

Mara tu ajali inapotokea ni muhimu sana kufata sheria maalumu ili kuhakikisha haupati usumbufu wakati wa kuomba malipo yako.

KWANZA: baada ya tukio hakikisha kuwa abiria wako wote wapo salama. Wasaidie kutoka nje ya gari ili kama kutakuwa na mafuta yanamwagika wasiwe kwenye hatari ya kulipukiwa.

PILI: Toa taarifa polisi. Mara nyingi maskari wa barabarani wanakuwepo katika maeneo mengi hivyo huweza kufika haraka kwenye eneo la tukio.

Kama hakuna askari karibu basi uliza watu waliokaribu kama kuna kituo mahali pa karibu, au tuma dereva pikipiki akakutolee taarifa na kuwaleta eneo la tukio.

TATU: chukua ushahidi wa picha na ripoti ya polisi kisha wasiliana na customer care wa Uber kwa kufata njia zilizochambuliwa kwenye makala ifuatayo:

Wasiliana na uongozi uber kwa kufata hatua hizi

Au kama hauna shida ya kuongea na mtu wa Uber basi unaweza kutoa taarifa ajali kwenye app yako kwa kwenda kwenye kipengele cha Help, halafu Trip issues and adjustments halafu I was in an accident.

Au unaweza kutuma ripoti hapa

JE UNAHITAJI HUDUMA HII?

Kama ulivyoona faida za hii bima ya ajali bure ni kubwa sana! Hasa kwa barabara za nchini kwetu ambazo zimejaa watu wanaoendesha kwa fujo kutokana na kuchoshwa na foleni.

Hata ukiwa dereva mzuri vipi ajali ni kitu ambacho hakiwezi kuepukika kwa 100%. Kwa hiyo kampuni ya Uber imefanya vizuri sana kuingia na kampuni ya bima ya Britam kuhakikisha kuwa madereva wote wanalindwa.

KAMA HAUTAKI BIMA YA MAJERAHA UNAWEZA KUIKATAA

Fuata link hii kuweza kupata fomu ya kujaza kama hautaki kupata fidia pale utakapopata ajali ukiwa unaendesha abiria kwenye Uber.

Je umewahi kupata ajali wakati ukiendesha Uber? Ulipata fidia zako zote? Tafadhali tushirikishe kwenye comment ili tuweze kujifunza kutoka kwako.

1 thought on “BIMA YA AJALI BURE KWA MADEREVA UBER WOTE TANZANIA”

  1. Pingback: UBER AU BOLT TANZANIA: IPI INAFAA ZAIDI KWA BIASHARA 2022? -

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *