Kama wewe ni dereva au mmiliki wa gari unayefikiria kutengeneza kipato kwa kutoa huduma ya usafiri basi umefika kwenye mahala sahihi. Katika makala hii utafahamu kama biashara ya Uber inalipa vizuri na kama inakufaa kuanza kutengeneza kipato full time au part time kwa kuendesha mwenyewe au kutumia madereva wanaohitaji magari ya kuendesha na Uber.
Uber ni nini?
Uber technologies au kama inavyofahamika sana kama Uber ni kampuni ya kimarekani ya usafirishaji yenye makao yake makuu jijini San Francisco California. Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2009 katika mji mmoja, lakini mpaka sasa huduma zake zinapatikana katika miji mikubwa zaidi ya 900 dunia nzima.
SOMA HAPA: Jinsi ya kujisajili kuwa dereva wa Uber 2022.
Mtiririko wa historia ya Uber
- Mwaka 2009 Uber ilizinduliwa kama UberCab na Garret Camp na Travis Kalanick
- Mwaka 2011 Uber ilianzisha shughuli zake kwenye jimbo la New York City
- Mwaka 2011 Uber ilianzisha shughuli nje ya Marekani ( Paris, Ufaransa )
- Mwaka 2012 Uber ilianzisha huduma katika jiji la London na ikazindua huduma ya UberX
- Mwaka 2013 Uber ilianzisha shughuli zake Latin America, China, India, Urusi, Nchi za mashariki ya kati na Africa
- Mwaka 2014 Uber ilizindua huduma ya UberPool na UberFresh
- Mwaka 2015 UberFresh ilibadilishwa jina kuwa UberEats
- Mwaka 2016 Uber China iliuzwa kwa Didi Chuxing (kampuni ya usafiri pia)
- Mwaka 2017 Dara Khosrowshahi akachukua uongozi wa Uber baada ya Travis Kalanick kumaliza muda wake
- Mwaka 2017 Uber ilizindua huduma ya Uber Freight
- Mwaka 2018 Uber ilizindua huduma ya Uber Cash, Uber Pro, Express pool na Uber rewards
- Mwaka 2019 Uber ilinunua Careem ambayo ilikuwa kama Uber ya Uarabuni iliyozinduliwa Dubai.
- Mwaka 2019 Uber ilizindua Uber Freight katika bara la Ulaya
- Mwaka 2019 Uber ikawa wazi kwa watu wengine kununua hisa na kuwekeza.
Watu wangapi wanatumia usafiri wa Uber duniani?
2015 | Milioni 11 |
2016 | Milioni 37 |
2017 | Milioni 68 |
2018 | Milioni 91 |
2019 | Milioni 111 |
2020 | Milioni 93 |
Kampuni ya Uber inatengeneza fedha kiasi kifuatacho kila robo mwaka?
Kampuni ya Uber ilizinduliwa lini Tanzania?
Uber Tanzania Limited ilianza shughuli zake Tanzania mwezi Juni mwaka 2016 kama kampuni ya kwanza ya Ride-sharing nchini hapa. Kutokana na TAFITI HII mwaka 2019 kulikuwa na zaidi ya madereva Uber 1,000 nchini Tanzania.
Hadi mwaka 2020 namba hiyo imesemekana kuongezeka mara mbili yake huku madereva wengi wakiwa ni madereva taksi walioweza kutambua haraka faida za jukwaa hili na kuhamia huko.
Hadi mwaka huu 2022, Huduma zinapatikana kwenya mji mmoja tu Tanzania ambao ni Dar es salaam.
ZIFAHAMU OFISI ZOTE NA NAMBA ZA SIMU ZA UBER TANZANIA
Maeneo yapi yana wateja wengi zaidi wa Uber Dar es salaam?
- Kariakoo
- Post Mpya
- Sea View
- St. John University
- Upanga
Biashara ya Uber inalipa kiasi gani?
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza madereva wa Uber Tanzania wanatengeneza shilingi ngapi kwa kila safari kwa siku au kwa mwezi. Swali hili si rahisi sana kulijibu kwasababu yapo mambo mengi sana yanayosababisha kipato cha madereva kuwa tofauti tofauti.
Ili kujua kama biashara ya Uber inalipa ni vizuri kufahamu makadirio ya malipo. Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika awali inasemekana kwamba wastani wa bei ya safari moja ni tsh 6,034/=.
Kwa wastani madereva wa Uber wanaweza kutengeneza mara mbili ya kiasi hicho ndani ya lisaa limoja yaani 12,068/=tsh kwa saa.
Kwa kuzingatia na kanuni hiyo, madereva wanaoendesha masaa 30 tu kwa wiki yaani kama masaa 4.5 kwa siku basi wanatengeneza kiasi kifuatacho kwa wastani:
- Tsh 362,040/= kwa wiki (Shilingi laki tatu elfu sitini na mbili na arobaini)
- Tsh 1,448,160/= kwa mwezi (Shilingi milioni moja laki nne elfu arobaini na nane na mia moja sitini)
- Tsh 18,826,080/= kwa mwaka (Shilingi milioni kumi na nane, laki nane elfu ishirini na sita na themanini)
Kumbuka hii ni wastani tu, wapo wanaoendesha masaa mengi zaidi na kupata pesa nyingi zaidi. Pia wapo wanaofanya kwa masaa machache zaidi na kutengeneza kidogo zaidi.
Huduma zipi za Uber zinapatikana Tanzania?
Kama tulivyoona hapo mwanzo Kampuni ya Uber ina aina nyingine ya usafirishaji ambazo ni kama nyongeza au mboresho wa huduma original ya kusafirisha mtu mmoja.
UberX
Hii ni huduma ya Uber inayoruhusu hadi abiria wanne kupanda gari moja. Hii ndiyo huduma inayopendwa zaidi kwasababu watu wengi hupenda kusafirishwa kwa vikundi kwa mfano wanafamilia.
Bei / Gharama za UberX
Huduma Nauli ya Zamani | Nauli Mpya | |
Nauli Msingi TZS 900 | TZS 1000 | |
Kwa kila Kilomita TZS 350 | TZS 400 | |
Kwa kila Dakika TZS 60 | TZS 72 |
UberConnect
Hii ni huduma ya kusafiria mizigo au bidhaa kwa watu binafsi au wateja wa wafanyabiashara. Huduma hii ilizinduliwa Tanzania tarehe 17/05/2021 na inafanywa na madereva wa UberBODA kwa hiyo gharama yake ni sawa na ya UberBODA.
Bei /Gharama ya UberConnect
Base fare | Tsh 700/= |
Kwa kilometa | Tsh 250/= |
Kwa dakika | Tsh 55/= |
Nauli ya chini | Tsh 1000/= |
Masharti ya UberConnect
- Mzigo hautakiwi kuzidi kilogram 15 kwasababu chombo cha usafiri ni boda boda.
- Thamani: mzigo hautakiwa kuwa na thamani ya zaidi ya tsh 115,000/=
- Bidhaa zisizoruhusiwa ni kama zifuatazo:
- Bidhaa haramu.
- Bunduki, silaha, na vipuri vya silaha.
- Pombe, madawa ya kulevya au bidhaa za tumbaku
- Vyakula au vinywaji vinavyoharibika haraka (kama mayai).
- Bidhaa hatari au zenye madhara mabaya, ikiwa ni pamoja na vilipuzi, bidhaa zenye sumu au zinazowaka moto rahisi, uchafu wa hospitali na bidhaa nyingine ambazo zina madhara kama inavyoainishwa na sheria husika.
- Pesa, kadi za zawadi (gift cards), tiketi za kamari au hisa zinazohamishika.
- Vitu/ bidhaa za wizi.
- Vitu ambavyo vinaweza kuvunjika kwa haraka kama glass.
Soma zaidi kuhusu UberConnect kupitia website ya Uber.
Huduma za Uber ambazo hazipatikani Tanzania ni kama zifuatazo:
- Uber XL : Hii ina uwezo wa kusafirisha abiria hadi 7.
- UberFreight: Hii inaunganisha makampuni ambayo yana bidhaa/mzigo na makampuni ya kusafirisha mali hasa kwenye malori makubwa.
- Uber Select, UberBlack na Uber SUV: Hii ni huduma ya Uber ya magari ya kifahari.
- UberPool: Inatoa usafiri wa pamoja kwa abiria tofauti wanaoelekeza sehemu moja.
- UberEats: Kwa ajili ya kuagiza na kuletewa chakula.
Kwa kifupi biashara ya kuendesha abiria wa Uber lina uwezo mkubwa sana wa kufanya mtu yeyote mwenye vigezo atengeneze kipato kikubwa sana. Na uzuri wa yote, hauhitaji kuwa unamiliki gari lako mwenyewe, na kama unalo gari si lazima uliendeshe mwenyewe.
Unaweza kuingia makubaliano na dereva ukamkodisha gari lako kuendesha na Uber na akatumia kiasi anachokipata baada ya kuendesha na Uber kukulipa mmiliki wa gari kiasi mlichokubaliana katika muda mliokubaliana.
Je umejifunza kitu kutoka kwenye makala hii?. Tafadhali tuambie kwenye sehemu ya komenti ni kitu gani kipya umepata.
Pia usisahau kushare makala hii na wengine wapate kujifunza kitu kipya!
Pingback: JINSI YA KUTENGENEZA PESA NYINGI KWENYE UBER/BOLT %
Mimi ni dereva ila sina gari pia nimevutiwa na program hii je naweza kunganishwa na mmiliki wa gari ili niweze kuendesha na uber??
Habari Francis!
Tumefurahi kama umevutiwa na huduma tunayotoa kupitia ukurasa wetu.
Ni nia yetu kuendelea kutoa msaada kwa watu wenye shida kama yako ili mpate nafasi ya kujitengenezea kipato cha uhakika kupitia biashara hii.
Endelea ku-subscribe kwenye ukurasa wetu, ili uendele kupata taarifa zitakazo kusaidia katika kutatua changamoto yako.
Asante.
Kiukweli airipi uber garama zake nikubwa Manaton yke makubwa abilities 29 kweli siopoa wateja awajawai kuwambia kua atuna ela mimi nimiliki wamagar matat uber nanishawai fanya mwenzi mmoj nilikuwa likizo kikazi hila magar yote nishatoa bei za uber na bolts nindogo sana mna Nyanza vijana waliowajili hila mkipunguza nakoto yenu ya abilities bc kdgo tuu
Makato ya uber na bolts nimakubwa sana vijana mnawatesa vijanamno hilo swala litafika hila endeleeni
Mi ni dereva ,imefika wakti sipendi na nachukia kubeba habilia wanao tumia kadi,kwa sababu taku nianze kubeba sikuwai kukuta pesa zangu kwenye Account yangu ya bank;na nikicheki kwenye wallat ya app,nakuta Hamna,inaniumiza sana.
Mimi kama dreva Uber na bolt kunamamboningependa yasiwepo kwamfano ofa hili swala la ofa linatuumiza madereva sana sasa basi kama ninyi mnato ofa nasisi tunatak hio ofa isiwepo kwenye deni iwekwe pembeni ili nasisi tuwadai zile pesa za ofa maana mnatoa ofa halafu zile garama za ofa mnazichuku mnaziweka kwenye den mnatuumiza hivyo hivyo kwenye cadi hakuna kuiweka kwenye deni wekeni pembeni nasisi tuone hela zetu za ofa na cadi
Habar.
Mimi ni dereva ni mzoefu wa kuendesha gar za mtandaoni na zinginezo ivyo naitaji gari ya kufanyia kazi mtandaoni kama uber.bolt.moovin.paisha.ping.little.indrive.na mitandao mingine kama gari lipo naomba unitafute kwa namba izi 0718503369