Watu wengi wanaotaka kuanza kuendesha abiria Uber hujiuliza sana kuhusu aina za magari zitakazofaa katika kuleta faida kubwa zaidi kwenye biashara hii ya usafirishaji.
Hii ni muhimu kwa madereva ambao tayari wanaendesha abiria wa Uber/Bolt/Linkee au kwenye majukwaa mengine kwasababu, dereva anaweza kubadili gari muda wowote na kuweza kutengeneza pesa zaidi.
Kabla ya kujua magari yanayofaa zaidi kwa kuendesha abiria, ni muhimu kufahamu aina ya magari yanayokubaliwa kusajiliwa Uber kwa KUSOMA HAPA.
AINA ZA MAGARI YANAYOFAA ZAIDI KWA UBER TANZANIA 2022
1. TOYOTA VITZ
Madereva wengi sana wanatumia aina hii ya gari katika kusafirisha abiria kwenye majukwaa ya usafiri kama Uber, Bolt, Linkee nk. Aina hii ina bei nzuri, inatumia mafuta kidogo na model nyingine zina muonekano fulani kama wa magari ya mashindano ambao huvutia watu wengi.
Toyota Vitz zina tanki la mafuta zenye ujazo wa Lita 42 na utumiaji wake wa mafuta ni Lita moja kwa kila Km 18 – 21.8.
2. TOYOTA IST
Hii ni moja kati ya aina ya magari yaliyopo kwa wingi zaidi Tanzania. Hii ni kwasababu bei yake ni nzuri sana na utumiaji wake wa mafuta ni mdogo. Lita moja ya mafuta inaweza kupeleka gari umbali wa Km 11.5 na tanki la mafuta lina uwezo wa kujaza Lita 42 za Petroli.
Ukilinganisha Toyota IST na Toyota Vitz, yote yana size nzuri, yanatumia mafuta kidogo na idadi ya siti ni sawa lakini, Vitz hutumia mafuta kidogo zaidi. Hii inamaanisha kuwa aina hii ni nzuri sana kwa ajili ya biashara ya usafiri kwasababu dereva anakuwa na gharama ndogo ya uendeshaji gari hivyo kupelekea faida kubwa zaidi.
Lakini ukilinganisha kwa kutumia kigezo cha starehe au comfort, Toyota IST zina nafasi kubwa zaidi ya Toyota Vitz. Kwa hiyo abiria warefu wanaweza kupata shida kidogo kwenye vitz kuliko kwenye IST. Kingine ni kwamba Toyota IST zina nafsi kubwa zaidi ya sehemu ya kuwekea mizigo kuliko vitz.
SOMA HAPA kuona tofauti na uwiano wa toyota IST na Vits.
3. TOYOTA PASSO
Aina nyingine ya gari dogo na linalopendwa kutumiwa na madereva katika majukwaa ya ride hailing ni Toyota passo. Size yake ndogo muonekano ni mzuri na ni rahisi kuegesha sehemu yoyote. Size na muundo mzima wa aina hii ya toyota husaidia matumizi madogo ya mafuta hivyo kuongeza uwezo wa kupata faida kubwa zaidi katika biashara.
Lita moja ya mafuta inaweza kuendesha gari aina ya Toyota Passo kwa km 20.8. Na model nyingi zina tenki la mafuta lenye uwezo wa kujaa Lita 40.
4. TOYOTA COROLLA SPACIO
Aina nyingine ya gari dogo lenye muonekano mzuri na nafasi ya kutosha ni toyota spacio. Magari haya pia yapo mengi sana kwenye majukwaa ya ride hailing Tanzania kwasababu yanapatikana kwa bei nzuri.
Ukilinganisha na aina tulizoongelea hapo juu, aina hii ni kubwa zaidi na inaweza kubeba abiria hadi watano. Siti mbili za nyongeza zinaweza kuwa ndogo kwa abiria watu wazima ila ni nzuri kwa watoto.
Spacio zina ukubwa wa injini wa 1,496 cc ambao umepitiliza kiwango cha juu cha Uber cha 1,300 cc. Hivyo aina hii ya gari inaweza kutumika kwenye majukwaa mengine kama Bolt kwasababu wao kima chao cha juu ni 1,500 cc.
Ukilinganisha na Toyota Raum, spacio zipo juu zaidi kwa umbali wa mm 165 kutoka chini wakati Raum in umbali wa mm 150. Tofauti hii ni muhimu sana kwasababu abiria wengi wa kwenye majukwaa haya ya usafiri huishi sehemu zilizopo nje ya barabara za lami ambapo kuna mashimo na mabonde.
Gari ambalo lipo chini sana linaweza kuumia kirahisi wakati wa kufanya shughuli hivyo kupelekea uchakavu na hasara ya ufundi wa mara kwa mara.
Toyota corolla spacio zina tanki la mafuta zenye ujazo wa Lita 52 na utumiaji wake wa mafuta ni Lita moja kwa wastani wa kila Km 13.6.
5. TOYOTA RAUM
Aina hii ni ndogo zaidi ukilinganisha na Spacio hivyo pia bei yake ni ndogo zaidi. Ukubwa wa injini yake pia ni 1496 cc hivyo haziwezi kusajiliwa Uber (Lakini zinaweza kutumika kwenye majukwaa mengine ya usafiri).
Toyota Raum zinatumia petroli, tenki lake lina uwezo wa kujaza full lita 52 na utumiaji wake wa mafuta ni Lita moja kwa wastani wa kila Km 15.
SOMA HAPA: SOMA HAPA kuona tofauti na uwiano wa toyota Corolla spacio na Toyota Raum
CHANGAMOTO ZA KUTUMIA AINA ZA MAGARI TULIOYATAJA
Ingawa magari haya yana faida nyingi na yanafaa sana kwa biashara, bado zina mapungufu ambayo huenda kuyapelekea kupungua kwa ufanisi wake wa kutoa huduma.
1. MAFUPI
Sio safari zote za kwenye majukwaa ya kusafirisha abiria hutumia bara bara nzuri za lami. Watu wengi sana wanaishi maenesho ya mbali na bara bara kuu kwenye sehemu ambazo kuna mabonde na mashimo.
Magari haya maarufu ni mafupi, kwa hiyo huleta shida kwa dereva pia hukumbwa na uwezekano wa kuharibika mara kwa mwara kutokana na kugonga chini.
2. SIZE NDOGO
Moja ya sababu kuu inayopelekea magari haya kutumia mafuta kidogo ni uzito na size yake ndogo. Siti ya mbele inaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi kwa ajili ya kunyoosha miguu kuliko za nyuma ila haishauriwi kwa abiria kukaa mbele.
Kama abiria ni mrefu basi kuna uwezekano mkubwa sana wa yeye kubanwa miguu anapokaa siti ya nyuma. Hii husababisha baadhi ya abiria ku cancel safari wanapoona gari zilizopo ni mojawapo ya hizi. Badala yake husubiria gari kubwa zaidi ili kuhakikisha wanakaa kwa starehe.
Je, ni aina ipi ya magari unaona yanaendeshwa zaidi kwenye majukwaa ya kusafirisha abiria?
Mm Ahmed Jana saa 9 mchana nililiquest bolt kwenye mtandao ilikuja IST lakini ilikuja PASSO yenye plati no ya njano safari yangu ilisoma 14000 kutoka magomeni mpaka goba njianne lakini Chakushangaza mwisho wa safari dereva ananiambia imesoma 28000 kwenye simu yangu inasoma 25000 tumegombana Sana dereva ananiambia nimpe 20000 tuyamalize kama nikweli imesoma 25000 kwann atake 20000
Majibu naomba mnijibu kwa wassap no 0783646378 email yangu inasumbua
Pole sana bwana Ahmad.
Kama bado una details za dereva, unaweza kwenda kwenye kampuni husika na kuripoti hili suala na kulipwa fidia pia hatua nyingine zitafuata kwa dereva kama vile kufungiwa account.
kwa kawaida bolt huwa wanatuma risiti kwa email kila badaa ya trip hivyo basi kama bado unayo risiti ya trip basi hiyo pekee inafaa kabisa kuelezea suala lako.
Hivyo basi unachotakiwa kufanya ni kufikisha lalamiko lako moja kwa moja kwa watoa huduma wa kampuni husika.
Tumia link hii hapa chini kupata namna ya kuwasiliana na uongozi wa bolt.
https://weibakcarsharing.com/wasiliana-na-uongozi-bolt-tanzania-kwa-njia-zifuatazo/
Hm,.. amazing post ,.. just keep the good work on!