ABIRIA WATATA KWA MADEREVA WA TEKSI MTANDAO.

Madereva wanaotoa huduma ya usafiri kupitia aplikesheni za Teksi mtandao hukutana na abiria wengi wenye tabia zinazotofautiana. Wapo abiria ambao ni wastaarabu lakini wapo abiria ambao ni watata au wagomvi. Ni vigumu na sio vyema kwa madereva kubagua abiria ila wanachotakiwa kukifanyani ni kuwa wepesi kuwatambua abiria wanaowabeba. Abiria watata kwa madereva wa teksi mtandao ni moja ya changamoto kwa madereva.

Dereva anapaswa kuwatambua abiria wastarabu na watata au wagomvi na kutafuta namna ya kuwapa huduma bila ya kuingia kwenye hali ugomvi au mabishano. Wafuatao ni aina ya abiria wenye utata na mambo unayoweza kuyafanya pindi unapokuwa umewabeba.

  1. Abiria waliolewa kupita kiasi

Mtu alie chini ya shinikizo la pombe huweza kufanya vitu ambavyo asingeweza kufanya kama akiwa katika hali yake ya kawaida. Pombe upelekea baadhi ya watu kupoteza kabisa ustaharabu. Mara nyingi madereva hukutana na abiria walio katika hali hii kwenye maeneo ya starehe.

Kitu cha kwanza unachopaswa kufanya pindi unapokutana na abiria aliye katika hali ya ulevi ni kusoma mazingira na kufanya tathmini ya haraka kama utaweza kumudu changamoto. Kama utaona itakuwa ngumu kwako au unashindwa kuyasoma mazingira basi ni vyema ukahailisha hiyo tripu.

Kama utaendelea na kutoa huduma kwa abiria aliyekatika hali hiyo, basi unashauriwa kujitahidi kuwa mtulivu na kufanya kila kitu kwa ustaharabu wa hali ya juu huku ukitambua kuwa mtu au watu hao hawapo katika hali zao za kawaida.

Pia usibishane na mtu aliye chini ya shinikizo la pombe kwani hakuna kitu utakacho faidika nacho. Kwa kiasi kikubwa mabishani yatakayotokea yanaweza kupelekea ugomvi unaoweza kupelekea hasara kwako wewe dereva.

Kwa mujibu wa Alex Kimaro, dereva wa Teksi mtandao Dar es Salaam,

“Ninapokutana na abiria aliyelewa, huwa ninajaribu kupunguza hali ya taharuki kwa kuzungumza kwa utulivu au kuhailisha tripu ikiwa abiria anakuwa mtata sana. Ikiwa abiria anaendelea kuwa mtata/mkorofi, mawasiliano yanafanywa na mamlaka husika kwa msaada.”

2.Abiria Wabishi/Wajuaji.

Hata katika maisha yetu ya kawaida huwa kuna aina hii ya watu ambao uona kana kwamba wao wanajua zaidi kuliko wengine. Madereva pia huweza kukutana na watu wa namna hii. Watu wa namna hii huwa hawapendi au hawawezi kusikiliza maoni ya wengine bali wao hupenda kusikilizwa na hawapendi kubishiwa.

Madereva wanapokuwa kwenye mazungumzo na abiria wa namna hii, wanashauriwa kujitahidi kuwasikiliza na kuwa watulivu.

Madereva wanashauriwa kuepuka mabishano na abiria wa namna hii kwa ku kwepa mada zinazoleta ubishi kama vile mpira au siasa.

3. Abiria wenye uchovu au msongo wa mawazo.

Katika kazi yako kama dereva ni lazima utakutana na watu wa namna hii. Wapo abiria wanaotoka kwenye safari ndefu na wanakuwa na uchovu na wengine wanatoka kazini wakiwa na uchovu na mawazo. Mtu aliye kwenye hali hii ya uchovu au msongo wa mawazo uweza kuonekana kirahisi na ni vyema kwa madereva kuwa wepesi kusoma mazingira.

Mtu ambaye yupo kwenye hali hii mara nyingi huwa hawapendi usumbufu na mara nyingi huwa na hasira za karibu sana. Dereva unashauri unapokutana na abiria wa namna hii basi ujitahidi tu kutoa huduma inayopaswa kutolewa kwa mteja wako, na kama wewe ni mzungumzaji sana basi jaribu kufanya mazungumzo ya vitu ambavyo havitakuwa na kero kwa abiria wako.

Lakini kama ukiona anajitahidi kukwepa mazungumzo basi jitahidi kumpa nafasi yake ya utulivu ili aweze kupumzika au kutafakari jambo linalomsumbua wakati akiwa kwenye safari yake

Kwa mujibu wa John Mwakalebela, dereva wa Teksi mtandao,

“Wakati wowote ninapokutana na abiria mwenye tabia utata au ukorofi, huwa na jaribu kuwa mtulivu. Ikiwa abiria ataendelea kuwa mtata, kwa upole ninahailisha safari.”

Hawa ni baadhi tu ya abiria watata kwa madereva wa teksi mtandao. Katika yote dereva unashauriwa kujitahidi kuwa mtulivu wakati wote. Mabishano au ugomvi na abiria wako haitakufaidisha kitu chochote zaidi tu itakuharibia kazi yako.

Jitahidi zaidi kuweka mawazo yako katika kile kilichokupeleka barabarani ili utimize malengo yako na maisha yaendelee.

Endelea kutembelea Website ya Weibak Carsharing na kujisajili ili upate email kila makala mpya za uchambuzi na elimu ya biashara ya Teksi mtandao (Ride-hailing) zinazochapishwa.

Kwenye comments tushirikishe kama wewe umewahi kutana na changamoto ya abiria watata na njia gani ulitumia kuifanyia kazi changamoto hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *